Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona hiyo biblia inasema watu wote watafufuliwa siku ya mwisho, sasa hao wanaochomwa inamaana wamefufuliwa kabla sisi hatujafa
Unajua wazee wa kiyahudi walijichanganya sana katika utunzi wa biblia yao? ... .. .
maana waliandika ya kuwa siku ya kiama itapigwa parapanda wafu wote watafufuka(sijajua kama wale ambao watakua hai watauliwa kwanza?)... .. .ndipo mwana wa adamu ataketi upande wa kuume wa baba kuwahukumu makabila 12 ya israel, na wale wema wataenda peponi na wabaya motoni... .. .
Sasa sijajua hawa ambao wako motoni saivi hukumu yao imefanyika lini wakati bado hatujamuona mwana wa adam akiteremka katika mawingu.
Wanajichanganya tu, biblia Ina maswali mengi mno sema ndo hivyo hawaruhusiwi kuuliza
Imgia youtube halafu type jina la huyo dr... usikie balaa lake
Duu! Kwahiyo Mungu sikuhizi anapatikana YouTube? Kweli siku zinavyozidi kwenda ndivyo inavyothibitika kuwa hizi hadithi za uwepo wa Mungu ni kama drama tu
Nani kamu upload huko YouTube?? Acha masikhara. Ukisoma thread vizuri ni kwamba kwa mujibu wa huyo Dr. Aliweza kurekodi sauti kutoka kqenye hilo shimo ikisemekana inatoka kuzimu. So ukiingia YouTube na kutype jina la huyo Dr. Utaweza kusikia hizo sauti walizorecord.
Nimeiangalia hiyo video. Kuzimu ni wapi? Nini kinachothibitisha kuwa hizo sauti zinatoka kuzimu?
Huwa napasikia tu huko kuzimu sijawahi fika ila kuna mtu anapajua kama vipi nikuunganishe nae akupeleke??
Mwambie athibitishe kwanza uwepo wa kuzimu, eneo ilipo na kila kitu sio kuisikiliza hadithi tu
Mkuu Kabla ya Hapo,Hii thread yenyewe Iliyoitwa Makala Imejaa Uongo Mtupu.
Kwanza,Mwandishi anasema kuwa,Ilo Kundi la Wanajiologia walichimba shimo lenye kina cha 14.4 KM mpaka katikati ya Dunia
Lakina Dunia ina layers kuu 3,Mantle ndiyo layer ya katikati ya Dunia[katikati Mwa Dunia],Ambayo Ipo umbali wa 2900 KM kutoka kwenye surface
Sasa shimo la 14.4 KM,ambayo ni sawa na 0.002% ya 2900 KM linaweza kumfikisha Mtu Mpaka katikati Mwa Dunia?
Pia hao wanajiologia wanasema kuwa Joto la huko lilikuwa ni 1000C',Ambalo wanadai ni kubwa sana
Lakini in Reality,Joto katikati ya Dunia ni 2,200C' mara 2 ya Hilo waliloli Detect.
Pia wanadai kuwa walisikia sauti zikilia,Huu ndiyo Uongo wa Mwisho.
Biologically,Mwanadamu anasikia sauti zinazo Range kati ya 20HZ-20000HZ[Audibility range]
Sasa sauti katika Medium yenye 1000C' ina Hz kubwa sana inayozidi Range,mwanadamu hawezi kusikia
Nakubaliana nawe kuwa ni uongo mtupu. Pia hatuwezi kuamini kitu eti kwa sababu tu gazeti la Finland limeandika. Kutoka kwangu mpaka border ya Finland ni masaa mawili tu kwa gari, Nna uwezo wa kwenda maktaba flani ya Finland kutafuta hilo gazeti ila tatizo sijui kifinish ila iko siku ntalifanyia utafiti hili swala kwa undani. Siamini kama hii habari ni ya ukweli, nadhani ni ya kutunga tu. Au ameipakua kutoka katika mitandao ya kizushi ya Ulaya
Hakuna kitu kama hicho,Hizo ni Bogus claim tu
Kama ni kweli,science isingekuwa kimya Mpaka sasa
toka Mwaka 1989 mpaka Leo kila Mtu angekuwa anajua.