Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

SIKU AKIPATA ..SAWA KAMA NI HIVYO majigambo tupunguze,,na ushauri hewa tunaotoa hapa auna maana ..tuwaachie wenye timu kina MO Dewji watuamilie nani watamsajili maana hao ndio wanato pesa ...sisi hata kuwasuport kwa kwenda uwanjani hatufanyi..theni tunakuja hapa midomo mireeefuu kupendekeza majina..shame on you..

Pale Madrid ,,,mashabiki wanaweza kufanya kama hivi na timu ikatekeleza maana wanalipa kila kitu,,na pesa wanazo..Barcelona pia the same..ila ona Man United hawawezi maana mwenye timu na mtoa pesa ni mtu mmoja mwingine kama ilivyo hapa kwetu Simba SC..

Tukubali,,kuwa shabiki wa Simba na Yanga bila kuichangia timu yako ..kisha unakuja hapa unalalamika na kutoa mapendekezo huo ni ujuha na uzwazwa
 
Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Yaani Mkude aachwe sababu ya mechi ya Kagera. Huwezi kukumbuka kazi nzuri ya mkude kwenye mechi ya Nkana, AS Vita, Al Ahally na TP Mazembe pamoja na mechi ngumu za TPL za Prisons na Mbeya city?
Mechi na As Vita hakucheza tulikua nae jukwaani (alikua pembeni yangu) Labda kama unaongelea ile tuliyopigwa 5 ambayo mchango wa wachezaji wote ulikua wa hovyo sana.
 
Kila Fans akiwa na uwezo ndio raha zaidi maana tutafanya kila linalowezekana ili kufurahisha mioyo yetu,,hata tukimtaka Messi ni suala la yeye kukubali tu kuja Afrika,,ila pesa itakuwepo..yes pesa itakuwepo toka kwetu Fans...

Hao Al Alhly kadi yao ya uanachama kwa mwezi mtu analipia USD 150 sawa na Laki nne kasoro za kibongo..wapo wanachama zaidi ya 50000..piga hesabu ujue ni pesa ngapi wanaingiza hapo..hiyo ni kwa wanachama pekee.

ukija kwa mashabiki + wanachama wanaoingia uwanjani ..uwanja wao unaingiza mashabiki 80000..tuseme nako hawajai wanaingia mashabiki 40000 au chini ya hapo..kiingilio kwa mechi yao moja ni kwa kiwango cha chini pengine niUSD 30 piga hesabu ujue wanakusanya USD ngapi kwa game moja ...

Vyote hivyo ukijumlisha yanazifanya Kampuni za Kimisri na Afrika kwa ujumla kulipa mabilioni ya pesa kuweka nembo zao kwenye jezi za AL Ahly achilia mbali wale akina Friends of Al Ahly ambao kazi yao ni kununua goli la kila mechi timu yao inapocheza mechi kubwa na za kimashindano..


Brother ukijifikiria hivyoo..utaishia kujiona unastahili kuwa hivyoo na utabaki hapo hapo
 
Hahahaa.. kuna sehemu umesema mechi ya Simba na Mazembe mashabiki hawakujaa! Mimi nilikua uwanjani siku hiyo mpaka kufika dka ya 30 uwanja ulikua ume jaa fully. Sasa hivi unasema Manchester United mtoa pesa ni mmoja!! Kwa kutumia hizi kauli zako mbili nimegundua wewe siyo mtu makini unaweza sema lolote tu ili mradi kutetea agenda yako. Naomba tukubaliane kupishana kimtazamo na lengo la huu uzi liendelee. Nipo njiani kucheck game naomba na wewe ufanye hivyo usi ishie kulipia card tu.
 
Inaonekana wewe ni MO... uwe unaenda uwanjani mwenyewe basi tuone.
Na kwa uhakika tu hao waliochuja tunaowataja humu wengi wataachwa ili uvimbe upasuke.
 
You know nothing bro...game na Mazembe walijitokeza watu lakini hawakufanikisha kuujaza uwanja mzee baba..game ile iliingiza watu 46 elfu na kitu hivi...Man United anayetoa pesa nani kama siyo familia ya Glazer kupitia bodi ya utendaji chini ya Ed Wood? hukumbuki jinsi walivyokuwa wanabana kumpa pesa Jose za usajili msimu ulipita?hukumbuki tu mzee baba,,ile haina tfauti na Man City,Liverpool na klabu nyingi za Uingereza ambazo zinamilikiwa na familia ..tofauti na Spain ambapo ukiacha bodi za klabu wanachama wanaweza kupendekeza jambo lolote lile ata ikibidi usajili wa mchezaji.
 
Inaonekana wewe ni MO... uwe unaenda uwanjani mwenyewe basi tuone.
Na kwa uhakika tu hao waliochuja tunaowataja humu wengi wataachwa ili uvimbe upasuke.
Ndugu acha ushabiki maandazi..watachunjwa kwa kuzingatia report ya mwalimu ama watachujwa kwa kuzingatia hisia za kishabiki kama zako,,maana waliko kwenye bodi nako ni mashabiki kama wewe
 
Mkuu AKILI TATU ameshawahi kujiuliza kwa nini MO DEWJI hakwenda kuwekeza Lipuli au Ndanda akaja Simba?
Business man..pili shabiki..

kumbuka alianza na iliyokuwa Mbagala Market kabla hajaifanya Afrika Lyon ..why asingeenda Singida United kwao huko?
 
Kwanini mechi za mikoani watu wanaujaza uwanja??...wewe achana na mambo ya simba hayakuhusu yanayokuhusu ni ya huko kwa ombaomba fc
 
Ndugu acha ushabiki maandazi..watachunjwa kwa kuzingatia report ya mwalimu ama watachujwa kwa kuzingatia hisia za kishabiki kama zako,,maana waliko kwenye bodi nako ni mashabiki kama wewe
Ndio nakushangaa we unaumwa nini sisi kujadili timu yetu... Mbovu anaonekana wazi ,wewe umesema unamshangaa anaesema KOTEI atoke.. Kati ya Kotei na Chama unamchagua James je wewe ni kocha au Mo?!
Tunabadilishana mawazo tu na kujadili ya timu yetu ambayo ikifungwa tunaweweseka mbele ya watani zetu... Kutuzuia kisa hatuna ela ya kusajili ni ajabu.
 
Business man..pili shabiki..
kumbuka alianza na iliyokuwa Mbagala Market kabla hajaifanya Afrika Lyon ..why asingeenda Singida United kwao huko?
Jibu sawa kabisa.. Nafikiri tuko sawa now.
 
Kwanini mechi za mikoani watu wanaujaza uwanja??...wewe achana na mambo ya simba hayakuhusu yanayokuhusu ni ya huko kwa ombaomba fc
kwani hadi Dk Hii haujui kwa nini mechi za mikoni watu wanajazana vile???

ok nakusaidia..wanajazana kwanza kwa kuwa timu inafanya vizuri..pili wanajazana kwa kuwa wanataka kuwaona wachezaji ambao wanaifanya timu ifanye vizuri..laiti kama timu ingekuwa kama Yanga ..nakuhakikishia hakuna ambaye angekuwa na mzuka na kuina timu ikicheza...
 
aahh.sasa kwa uwongo mzee na mimi istoshe sijajitoa nipo kwenye kundi la lenu.lakini ukweli ndio huo,,kuwa hatuna hata pesa achilia tu ya kusajili mchezaji hata ya kulipa tu poshooo..sasa kama tunajua tuko hivi ya nini kudeal na vitu ambavyo hatuviweziii..tuhakikisheni kwanza tunautete ushabiki wetu then ndio tuwe na hizo hisia za kuzungumza kuhusu hii tunayoiita timu yetu
 
Jibu sawa kabisa.. Nafikiri tuko sawa now.
utofauti wake na wetu kaamua kuonyesha ushabiki wake wa kweli kwa kuamua kuwekezawewe na mimi tunakibali kipi cha kusema sisi ni mashabiki wa simba ? zaidi tujiite wapiga kelele wa simba maana hatuna tunachoichangia timu...maana hata hizo kelele heri tungekuwa tunazipiga uwanjani basi.tunazipiga nnnje kuwatambia watu baki
 
Jibu sawa kabisa.. Nafikiri tuko sawa now.
leo hii akiamua kuibadili jina timu..kwa kuwa anapesa ataitisha mkutano wa kikatiba ,pesa itatumika atabadili jina..rangi na jezi kabisa ...uzuri tushukuru hawezi kwa kuwa ni mwenzetu ila akiamua akasema nataka Simba iitwe Juvetus of Africa anaweza tuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…