GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Katika uzi wangu wa leo ambao pia nilijaribu kupanga vikosi vyangu viwili tofauti ambavyo niliona vingetupa matokeo na mwishoni, nilisisitiza mno kuwa mechi ya leo kwa uchezaji wa kutumia nguvu nyingi walionao waganda ingemfaa sana na angeisaidia Simba SC kimchezo.
Huhitaji kupoteza muda au kubisha kuwa kama kuna mchezaji wa Simba SC ambaye leo amejitoa na amepambana kwa nguvu zake zote kuipambania Simba SC hadi tone lake la mwisho ni Kibu Denis (Kibunenga).
Kwa takribani dakika 80 alizocheza leo Kibu Denis aliweza kushambulia, kukaba, kusumbua mabeki wa Vipers FC huku akihaha karibu uwanja mzima hali iliyowafanya wachezaji wavivu (ila kwa unafiki wetu) hatuwasemi (japo leo wameharibu mno) akina Clatous Chama na Saido Ntibanzokinza wapumue na wasikabe pia.
Bado sijaona shida ya kihivyo ya Kibu Denis isipokuwa naona tu kuwa ana nyota ya kuchukiwa bila sababu za msingi na mashabiki wa Simba SC kwani kama ni kuwa na mapungufu Pape Sakho ana mapungufu mengi ya kumzidi isipokuwa tu magoli yake ya kipekee na yanayompa tunzo ndiyo yanamfunika asisemwe au asichukiwe ila hana msaada kwa timu kama alionao Kibu Denis.
Nikiwa kama psychologist kitaaluma na wa asili ninachokiona tu ni kwamba endapo mashabiki wa Simba SC (hasa wale wanaomchukia na wasiojua mpira) siku wakimkopa tu imani yao Kibu Denis na yeye pia atawalipa ufanisi wake wa 100% uwanjani na kama GENTAMYCINE nina imani nae kubwa mno na hayuko mbali kutufunga midomo yetu kwa mpira wake mkubwa na wenye msaada mkubwa kwa timu tofauti na anavyochukuliwa na wengi.
Hongera Simba SC, hongereni wana Simba SC kwa ushindi wetu muhimu huko Kampala nchini Uganda dhidi ya Vipers FC na asante sana na mno mchezaji Kibu Denis kwa kujitoa kwako kwa nguvu zako zote ili kuipambania Simba SC kwa mchezo wa leo na hata kwa mechi dhidi ya Azam FC ambayo tayari Simba SC tulikuwa tunaenda kuumbuka na kutafutana uchawi.