Wana Yanga hebu nunueni tiketi za mchezo wa Al Hilal

Wana Yanga hebu nunueni tiketi za mchezo wa Al Hilal

Tena mimi nataka tupoteze sasa, viongozi wajifunze kufanya maamuzi kwa busara.

Hersi sifa zimempanda kichwani, bado sioni kosa la kuondolewa Gamondi.
Hakika sifa zimemzidia adi anaanza kuharibu, Gamondi hata kama angeondolewa haikupaswa kuwa wakati huu.
 
Nimemsikia akisema siku 6 hazitoshi kwa kocha yeyote yule duniani.

Lakini hilo sijui kama wanajali waajiri wake. Sidhani kama wana huo uvumilivu wa kupoteza mechi mbili na bado wakaendelea kubaki na kocha.
Ngoja tuone hii german machine itatupa nini cha kumzidi gamondi, na huyu akipoteza mechi kadhaa zijazo anaweza akauona mwaka mpya kwa taabu sana.
 
Huu ni msimu wa 3 sijawahi kukosa mechi yoyote ya Yanga ya kimataifa hapa nyumbani ila hii sitoenda, uamuzi wa kumfuta kazi Gamondi umenikera sana.

Timu ikishinda sawa, isiposhinda sawa pia.
Kamfate Gamondi huko alipo achana na Yanga tuone kama kuna kitu utakipunguza
 
Tena mimi nataka tupoteze sasa, viongozi wajifunze kufanya maamuzi kwa busara.

Hersi sifa zimempanda kichwani, bado sioni kosa la kuondolewa Gamondi.
Kumbe wewe ulikuwa unampenda mtu na sio timu, sasa Gamondi kafukuzwa na moto ndio unawashwa tena ni kama betri linalochajiwa na upya baada ya charge kuisha. Uchawi wako na unafiki wenu mtashushuka, aliyemleta Gamondi ndio huyo huyo aliyemleta Saed.
 
Back
Top Bottom