Wana Yanga SC hebu 'tuchangishane' upesi 'tukamlipie' Msemaji wetu Hassan Bumbuli 'Faini' yake TFF kwani GSM na Injinia Hersi ni kama 'wamemtosa' vile

Sitaki kuamini kuwa ni kweli hiyo faini haijalipwa TFF na yeye mwenyewe Bumbuli au klabu yake. Kiukweli kama yeye hakuwa na uwezo wa kulipa ilipaswa waajiri wake Yanga wamlipie. Iwapo waajiri wake hawajalipa basi ni kwamba hawamtaki kwa hiyo Bumbuli akatafute shughuli nyingine sasa. Kwa upande mwingine nitamlaumu sana Bumbuli iwapo alikosa pesa ya kulipa faini halafu akakaa kimya wakati Yanga ina mashabiki mamilioni ni kiasi tu cha kuondoa aibu na kuwaambia ukweli kuwa hana milioni 5 za faini na zingechangwa ndani ya dakika kumi tu kupitia mitandaoni.
 
Siku zote viluilui wakiwa kwenye dimbwi la matope wanarundikana pamoja na kuwa na mshikamano wa kuchezea tope, mmoja akipatwa na tatizo tu.....wengine wote wanakimbila kutoka ndani ya maji kuja nje kutafuta maji mengine, matokeo yake wanakwama mchangani na kukauka na jua kwa kukosa maji na hivi ndivyo viluilui wa Jangwani walivyo. Kelele nyingi mtandaoni ila wakipatwa na tatizo wao ni kulia tu lakini kuchangiana kwa jambo la maana hawataki.
 
Yanga wanadai pesa ya Tambwe, Dante zote hawajalipa halafu utegemee wamlipie bumbuli sahau hiyo kitu
 
Bumbuli angekua wa muhimu pale Yanga angeshalipiwa.
Hiyo ni pesa ya kawaida kwa mwajiriwa wa Yanga, Simba kuanzia mpate bwana wa kihindi mjini mnatembea vidole juu mkiwaza kulipiwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…