BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Kukubali ukweli siku zote siyo udhaifu bali ni sehemu ya kujisahihisha. Ukweli ni kwamba USM Algers siyo TP Mazembe, Marumo Gallants, Rivers Wala Monastry. Wakati mwingine ni ngumu kwenda vitani huku ukiamini kuwa hutarejea, lazima ufe, ila uamini usiamini ukweli utabaki kuwa kurudi kwako ukiwa hai ni % ndogo sn.
Kwa hili Wananchi na viongozi kujiaminisha kwa 💯% kuwa lazima mrudi na kombe ktk mechi ya leo ni sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenye. Mwisho wa siku matamanio yetu yanaposhindwa kufikiwa ndiyo utaskia flani kafa kwa pressure, mara kiongozi flani hafai atupishe au kocha huyu siyo wa kimaifa, level zake ni Mbeya City nk.
Wananchi kujiandaa kisaikolojia nayo ni njia sahihi ya kutibu ugonjwa wa akili. Kulileta Tanzania kombe la shirikisho kwa mechi ya leo ni zaidi ya maajab ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
NB:,
Heri kufa kiume kuliko kufa kikondoo.
Tukutane saa 4:00 usiku.