Wana Yanga wachukizwa na kauli ya Hersi kuhusu TFF

Wana Yanga wachukizwa na kauli ya Hersi kuhusu TFF

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Siku zote tunawaambia wanayanga kwamba Hajj Manara ndiye mwenye uchungu na team hiyo anayoipigania kwa moyo mmoja bila kujali maslahi ya pesa

Kitendo cha kuweza kuvitoa virusi sugu viitwavyo Nugaz na Bumbuli hapo klabuni vimemuongezea credit sana kwa wanazi wa yanga, jinsi alivyompa makavu Karia kule Arusha ilidhihirisha ni mwanajeshi kwelikweli aliye tayari kuipigania klabu yake hiyo ya utotoni

Sasa baada ya visa vyote vya Tff kumfungia Manara, kusimamisha biashara yake ya pafyumu, kufungia wachezaji wa yanga hovyohovyo bado Rais Hersi anasema hawana shida na TFF? kweli jamani?

Haya, wewe endelea tu utakipata unachokitaka, mitaa imekasirika inasimama na Jenerali Manara maana hata ahadi yako ya kujenga uwanja wa kisasa pale jangwani ushaanza kuichengesha


1.JPG
2.JPG
 
Siku zote tunawaambia wanayanga kwamba hajj manara ndiye mwenye uchungu na team hiyo anayoipigania kwa moyo mmoja bila kujali maslahi ya pesa

Kitendo cha kuweza kuvitoa virusi sugu viitwavyo Nugaz na Bumbuli hapo klabuni vimemuongezea credit sana kwa wanazi wa yanga,jinsi alivyompa makavu karia kule Arusha ilidhihirisha ni mwanajeshi kwelikweli aliye tayari kuipigania klabu yake hiyo ya utotoni

Sasa baada ya visa vyote vya Tff kumfungia manara, kusimamisha biashara yake ya pafyumu,kufungia wachezaji wa yanga hovyohovyo bado Rais Hersi anasema hawana shida na Tff ? kweli jamani?

Haya , we endelea tu utakipata unachokitaka, mitaa imekasirika inasimama na Jenerali manara maana hata ahadi yako ya kujenga uwanja wa kisasa pale jangwani ushaanza kuichengesha


View attachment 2366850View attachment 2366852
Hersi ana elimu. Ninyi ambao hamna Elimu ndo mnakuwa hivi.
 
Anawasifia maadui wa yanga? Mungu ambariki sana bugatti kwa upendo wake wa dhati kwa yanga sc
Huyu haris kiufupi anatuhujum kwanza hamfikii elim bugatti pili CV ya Bugatti ni kubwamno ndani ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.Kiufupi CV ya manara imekita mizizi dunia nzima

Nb
Mim kama mwanayanga tena mwanachama hai naomba Bugatii apewe iyo nafasi
 
HERSI SAID AMEANZA KUJIELEWA.

MANARA NI KIRUSI. CHUKI ZAKE BINAFSI KWA WATU HUWA ANAZIHAMISHIA YANGA.

KABLA MANARA HAJAHAMIA YANGA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA TULIKUWA WATANI WA JADI ILA SASA HIVI NI MAADUI HADI MATUSI YA NGUONI YAMETAWALA.

SOKA LETU LINAENDA WAPI? UPENDO WETU KAMA WATANI WA JADI UMEYEYUKA!
 
Chawa on air. Uwezi kushindana na mamlaka hata cku moja.
 
Back
Top Bottom