Chombo cha Starliner kilichoundwa na kampuni ya Boieng hatimae kimeweza kuaondoka kutoka kituo cha anga cha ISS lakini bila kuwabeba abiria wake wawili kutokana na hofu za kiusalama baada ya chombo hicho kupata hitilafu tangu kiwasili huko.
Wanaanga wawili wa kimarekani mmoja mwanamume aitwaye Butch na mwengine mwanamke aitwaye Sunni Williams wataendelea kubaki kwenye kituo hicho mpaka mwezi Februari mwakani ambapo chombo kingine cha Space X kinatarajiwa kupelekwa kuwarudisha nyumbani.Wanaanga hao tayari wameshakaa muda mrefu huko kinyume na muda waliopangiwa kukaa.
View attachment 3089237