Gentleman kua mkweli basi hata kidogo tu,
sijisufii ila angalau nina siha njema na bongo kali,
siwezi na sintaweza kua na mihemko wala kuthubutu kumporomoshea mwananchi yeyote matusi katika jukwaani hili lililosheheni wadau wabobevu na wa heshima sana kwangu,
ila nikiri tu kwamba,
nina udhaifu na mapungufu katika kujizuia na kukudhibiti katika kusema ukweli bila woga wala kificho.
Hata hivyo, siwezi kamwe kujifunza uongo na upotoshaji.
niwie radhi kwa hilo gentleman,
Hata hivyo,
tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, nichukue fursa hii kukuomba msamaha wewe binafsi
econonist na wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine huenda kupitia hoja, makala, maelezo au ufafanuzi wangu uliwakwaza.
ni matumaini yangu,
tunapoelekea mwaka mpya 2025, ambao pia ni mwaka wa uchaguzi, tutakua na mijadala muhimu ya kistaarabu zaidi kwa maslahi mapana ya ustawi wa demokrasia ya Taifa letu.
nakutakia maandalizi mema ya Christmass na heri ya mwaka mpya 2025 in advance.🐒
Mungu Ibariki Tanzania