Wanachama wa vyama vya siasa na wadau wa siasa kwa ujumla acheni mihemko, mizaha na matusi kwenye mijadala yenye maslahi muhimu kwa taifa

Wanachama wa vyama vya siasa na wadau wa siasa kwa ujumla acheni mihemko, mizaha na matusi kwenye mijadala yenye maslahi muhimu kwa taifa

gentleman,
nadhani una hoja mahususi unajaribu kuijenga na kutaka kuitoa, lakini nadhani ingefaa zaidi ingejitegemea.
hata hivyo haidhuru,

ikiwa hoja na maelezo yako yakawekwa kwenye mpangilio na mtiririko rasmi, wadau wasiofahamu chochote kuhusu hilo wangepata kujua, kuelewa na kuongeza ufahamu na uelewa wao juu ya jambo lenyewe,
na ndiyo maana nasisitiza ustaarabu katika kuwasilisha mijadala lakini piakujadiliana mambo mbalimbali ili hatimae tuwe na uelekeo na hitimisho la amani hata kama hatujakubaliana mawazo, maoni na mtazamo.

Mungu Ibariki Tanzania:pulpTRAVOLTA:
Kama yupo hawezi kuibariki na ndio maana tunatekana.
 
Kuweni wastahimilivu na wenye subra ikiwa hoja, mitazamo, maoni na fikra tunduizi za wadau kwenye masuala mbalimbali ni nzito, za maana na muhimu zaidi ya mawazo, maoni au mitazamo yenu ambayo labda ni dhaifu na yasiyo na mashiko kwa wakati huo.

Ikiwa umefikia ukomo wako wa mwisho wa mawazo mapya na fikra mbadala, huna sababu hata moja kulazimisha hoja au kuhitimisha maoni yako dhidi ya mjadala mahususi jukwaani kwa kuporomosha dhihaka, kejeli na pengine matusi ya nguoni kwa mtoa hoja au wadau na wachangiaji wengine.

Tumia haki na uhuru wako wa kujieleza kwa staha na kuchochea uhai na afya ya mijadala ya kistaarabu ili hatimae kwa pamoja tujenge Taifa au jamii iliyostaarabika na yenye kuheshimiana.

Hekima ikuelekeze kukaa kimya, ama kuperuzi mada nyingine kwenye majukwaa mengine kujiliwza kidogo au kuchukua nafasi ya kupumzika kidogo ikiwa utakua umejiskia kuchoka kulingana na uwajibikaji wa majukumu mbalimbali ya kila siku.

Kua mstaarabu mwenye weledi na bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.

Aidha nawatakia wadau wote wa JF utulivu na maandalizi mema katika mapumziko ya sherehe za Christmass na mwaka mpya 2025.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Anza kujitambulisha wewe ni wa chama gani,ili tuende sawa.
 
Gentleman kua mkweli basi hata kidogo tu,
sijisufii ila angalau nina siha njema na bongo kali,

siwezi na sintaweza kua na mihemko wala kuthubutu kumporomoshea mwananchi yeyote matusi katika jukwaani hili lililosheheni wadau wabobevu na wa heshima sana kwangu,

ila nikiri tu kwamba,
nina udhaifu na mapungufu katika kujizuia na kukudhibiti katika kusema ukweli bila woga wala kificho.
Hata hivyo, siwezi kamwe kujifunza uongo na upotoshaji.
niwie radhi kwa hilo gentleman,

Hata hivyo,
tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, nichukue fursa hii kukuomba msamaha wewe binafsi econonist na wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine huenda kupitia hoja, makala, maelezo au ufafanuzi wangu uliwakwaza.

ni matumaini yangu,
tunapoelekea mwaka mpya 2025, ambao pia ni mwaka wa uchaguzi, tutakua na mijadala muhimu ya kistaarabu zaidi kwa maslahi mapana ya ustawi wa demokrasia ya Taifa letu.

nakutakia maandalizi mema ya Christmass na heri ya mwaka mpya 2025 in advance.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Kwakuwa kazi uliyojipa ama kupewa ni ya kuwahadaa wale unaomudu kuwa hadaa.
 
Kwakuwa kazi uliyojipa ama kupewa ni ya kuwahadaa wale unaomudu kuwa hadaa.
gentleman,
sina haja wala sababu hata moja kuhadaa mwananchi kama wewe ambae ndio kwa kiwango kikubwa unanitegemeza. Huo utaku ni ukatili mbaya sana wa kisaikolojia.

hata hivyo,
ni hiyari kua mustaarabu na mwenye heshima kwenye mijadala, lakini sio lazima kuhasimiana eti kwasababu tu kuna utofauti wa mirengo ya kisiasa.

nakutakia Christmas njema na heri ya mwaka mpya2025 in advance, gentleman :pulpTRAVOLTA:
 
Anza kujitambulisha wewe ni wa chama gani,ili tuende sawa.
articles za wadau zinatambulisha mirengo ya vyama vyao kwa uwazi sana gentleman

huwezi kubabaika wala kupata mawenge kutambua nani ni nani wa chama gani katika siasa za Tanzania, huhutaji kuwa mbobevu wa chuo kikuu kwenye hili :NoGodNo:
 
gentleman,
sina haja wala sababu hata moja kuhadaa mwananchi kama wewe ambae ndio kwa kiwango kikubwa unanitegemeza. Huo utaku ni ukatili mbaya sana wa kisaikolojia.

hata hivyo,
ni hiyari kua mustaarabu na mwenye heshima kwenye mijadala, lakini sio lazima kuhasimiana eti kwasababu tu kuna utofauti wa mirengo ya kisiasa.

nakutakia Christmas njema na heri ya mwaka mpya2025 in advance, gentleman :pulpTRAVOLTA:
Hakuna tofauti ya mirengo na sina mrengo wowote japo ulio na haki wowote ule utakuwa mrengo wangu,ukitaka ueleweke zungumzia jambo kwa uhalisia,acha mahaba,acha hadaa hata na uongo wenye kunufaisha upande uliochagua,kwa maslahi ya nani hayo nakuachia mwenyewe.
 
articles za wadau zinatambulisha mirengo ya vyama vyao kwa uwazi sana gentleman

huwezi kubabaika wala kupata mawenge kutambua nani ni nani wa chama gani katika siasa za Tanzania, huhutaji kuwa mbobevu wa chuo kikuu kwenye hili :NoGodNo:
Hata huo mremgo wako ungekuwa ni wahaki ungenikuta humo
 
Hata huo mremgo wako ungekuwa ni wahaki ungenikuta humo
ni uhuru na haki ya kikatiba kwa kila mwananchi kua katika mrengo wa kisiasa amboa anaona unamfaa..

ustaarabu na kuheshimiana lazima paanzie hapa gentleman :pulpTRAVOLTA:
 
Ukiwa hujali utu utapopolewa tu ili ukae sawa
gentleman,
msingi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ni utu na usawa wa mwanadamu. Na huo ndio mwanzo wa siasa safi za ujamaa na kujitegemea Tanzania. Ukinunua kitu kwa pesa yako mwenyewe unashukuru kwa kusema asanti, ukipewa kitu au kusaidiwa jambo vile vile unashukuru kwa kusema asanti.

huo ndio ustaarabu na huko ndiko kuheshimu utu wa kila mtu na si vinginevyo.

Mary Christmas and happy new year in advance gentleman :pulpTRAVOLTA:
 
ni muhimu sana kumshukuru Mungu kwa kila jambo gentleman :pulpTRAVOLTA:
Mimi siwezi,nitachagua mambo ya kumshukuru.
Yaani na wale walioamua kwenda mbinguni na ndugu yetu JPM kwa hiyari yao nisishukuru kweli?

Ila hili la kuwafukuza wana Ngorongoro na kugawa malalio yetu kama zawadi kwa DP world siwezi kutoa shukrani kwakweli.
 
gentleman,
msingi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ni utu na usawa wa mwanadamu. Na huo ndio mwanzo wa siasa safi za ujamaa na kujitegemea Tanzania. Ukinunua kitu kwa pesa yako mwenyewe unashukuru kwa kusema asanti, ukipewa kitu au kusaidiwa jambo vile vile unashukuru kwa kusema asanti.

huo ndio ustaarabu na huko ndiko kuheshimu utu wa kila mtu na si vinginevyo.

Mary Christmas and happy new year in advance gentleman :pulpTRAVOLTA:
Utajua hujui we jichanganye tu, utayaoga
 
Mimi siwezi,nitachagua mambo ya kumshukuru.
Yaani na wale walioamua kwenda mbinguni na ndugu yetu JPM kwa hiyari yao nisishukuru kweli?

Ila hili la kuwafukuza wana Ngorongoro na kugawa malalio yetu kama zawadi kwa DP world siwezi kutoa shukrani kwakweli.
bas kua huru kumshukuru Mungu kadiri uonavyo inafaa gentleman 🐒
 
gentleman,
hoja yangu mahususi inasisitiza mno habari ya kujizuia na mihemko na kuupa kipaumbele utulivu na ustaarabu kujieleza, ambao kwakweli ni jambo muhimu na la maana sana katika kuwasilisha maoni na mtazamo wako juu ya mambo kadha wa kadha yanayotokea katika taifa letu.

Mihemko na ghadhab zinakufanya ukose utaratibu mzuri wa kujieleza na matokeo yake kuwapa kazi kubwa sana wadau kukuelewa. Lakini pia kwa kiasi unawakosesha fursa ya kujifunza kwenye maelezo yako yaliojaa ghadhab kuna jambo muhimu la kuongeza Ufahamu na uelewa wa wadau.

Tunapoelekea kuhitimisha mwaka huu 2024, ni muhimu kujipanga2025, kwa kuepuka mawenge katika kureply na kukomenti mambo mahususi kwa kuchanganya hisia ambazo ni artificial dhidi ya uhalisia na ukweli wa mambo.

Nakutakia maandalizi mema ya Christmass na happy new year 2025 in advance 🐒

Wewe nenda kwa machawa wenzako tuache sisi tupiganie nchi. Ustaarabu upi kwa hali hii yaani nchi iko kwenye ajali halafu tuwe na utilivu toa ndoto zako hapa tuache na minadala yetu. Is too late now! Hiyo treni imeshaondoka muda urasuburi sana hapa ni mwanzo tu mwaka kesho utulivu sahau gentle
lady
 
mihemko sio deal na sio ustarabu mzuri hata wa kufikia malengo binafsi tu gentleman, sembuse malengo ya jumla?

nadhani alie too late inaweza kua ni wew binafsi pekee. kwamba mwaka unaishi, hujatimiza lengo hata moja,eti sasa hivi ndio unachanganya miguu 🤣

that is too late,
relax na ujipange kwajili ya mwaka ujao gentleman.

kama taifa, kistaarabu kabisa tunajipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, baada ya kumaliza kwa mafanikio makubwa sana uchaguzi muhimu wa kihistoria wa serikali za mitaa.

ustarabu umefanya uchaguzi huo muhimu kua wa amani na Utulivu sana 🐒
 
Utaniambia mwaka kesho si unakuja! Hii nchi wanaigeuza kuwa radical polepole hata vyama tutaona viongozi radical zaidi na mimi sijasema hii ni nzuri lakini nachosema ni matukio ya chama tawala na serikali ndiyo yametufikisha hapa
 
Gentleman,
Kama mdau muandamizi katika siasa za Tanzania, mwaka ujao wa fedha na uchaguzi mkuu, utakua ni mwanzo wa mageuzi na mabadiliko makubwa mno ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika Taifa letu.

Tanzania inakwenda kuweka historia katika bara la Africa kwa kufanya uchaguzi mwingine ambao ni wa amani zaidi, pengine kuliko hata ule wa marekani katika ngazi za ubunge, udiwani na urasi.

Tujipange vizuri kama Taifa ndrugu zango 🐒
 
Changuzi mnazikuza tu hata huu uchafu uliopita unaitwa uchaguzi. Mimi naongelea hali halisi za watu na mambo tunayo yaona ground. Hizi chaguzi ni ratiba tu. Tanzania tuna dharaulika kuliko 2021 na 2022
 
Back
Top Bottom