Vema hata Mwandishi angesema tu " baadhi ya wanachama wa Yanga" ndio wamefanya hilo tukio badala ya kuandika kama vile wanachama walio wengi ndio wamefanya hivyo.Huu ushamb sijui utaisha lini??
Hivi wanachama wote wa Yanga kama wangeenda Jangwani hali ingekuaje?Mleta mada nawe unatatizo kubwa. Mbona hiyo heading ni kubwa kuliko tendo? Ati Wanachama wa Yanga. Mimi mbona sikuwepo wala sikushirikishwa? Gazeti lenyewe moja tena lililetwa ofisini bure halaf ndio limechanwa chanwa likawashwa na kiberiti cha sigara kali. Nayo hiyo ni hoja kweli ya kuandika humu jf?
Hata tungeshinda ingesaidia nini?JKT nae kabebwa awapakate?
Naona aibu kwa hii akili kwa sababu Na Mimi nashabikia yangaNilidhani wamewavamia wauza magazeti na kuyachoma,kumbe wameyanunua!!
Hili zoezi likiwa endelevu tena nchi nzima,Mengi atatengeneza pesa sana.
Nilidhani wamewavamia wauza magazeti na kuyachoma,kumbe wameyanunua!!Hili zoezi likiwa endelevu tena nchi nzima,Mengi atatengeneza pesa sana.
Mkuu wala usipoteze muda na hao wavamizi na waharibifu wa makazi ya vyura pale Jangwani.Mafisadi ni wajanja sana.
Wameshawanunua baadhi ya wanachama ili wahalalishe ufiasadi wao. Kama Cocobeach inamuhusu awajibike asijifiche nyuma ya Yanga wala CCM.
Na mwaka huu Magufuli akiamua kutenda haki sawa kwa wote wataikimbia hii nchi. Yanga ina tija gani kwa taifa kama itatumika kama kichaka cha mafisadi?
Club ni kwa ajili ya kuburudisha tu na sio kutumika kutuibia.
Kama kuna ukweli kwenye tuhuma hizo basi atumbuliwe.
Hii nchi tumebaki nyuma sana kwa mambo ya kipumbavu.
Mtu anatuhuma halafu anapanga watu wa kumpigia kelele .
Mara wengine wanatetewa kidini,wengine kikabila,wengine kikanda ,wengine kichama na kisiasa na sasa Wamekuja kisoka. Ajabu kabisa. Hao wanachama wananufaika nini endapo serikali itakua inahujumiwa na matajiri ili kufadhili vilabu?
Yani miundo mbinu ya Taifa iharibiwe ili kulinda mfadhili wa timu?
Je,siku akifa ina maana taifa letu ndio litaishia hapo?
Uko sahihi mkuu..ila ukweli Manji keshawaweza mapoyoyo wengi pale Yanga..ila kuna siku atawaliza..trust me ipo hiyo siku.Mengi ni shabiki wa Yanga na mfanyabiashara kama Manji. Hakukuwa na haja ya kuihusisha timu(brand ya Yanga) na ugomvi kati ya wafanaybiashara hawa wawili maana ugomvi wao upo bayana na ni wa muda mrefu. Manji hatakuwepo milele Yanga, hivyo si vizuri kuwafanyia fujo,dharau na kejeli wadau wengine wa Yanga kwa sababu ya Manji. Pia Manji atambue kuwa hao wanaopigana vita kwa niaba yake, ipo siku watapigana dhidi yake maana hawana maslahi na timu, bali mtu binafsi.
Kukosa ueledi katika masuala ya soka, ndio chanzo cha kudorora kwa timu zetu kimataifa. Tukatae kuharibu brand ya Yanga kwa maslahi ya mtu binafsi. Pamoja na mafanikio tuliyoyapata chini ya Manji, Yanga ni kubwa kuliko yeye. Manji si Yanga, wala Yanga si Manji.