Wanachama Yanga wachana na kuchoma magazeti ya Reginald Mengi!

Wanachama Yanga wachana na kuchoma magazeti ya Reginald Mengi!

Tatizo kubwa sana ni elimu.

Hata common sense hawana.
 
Ni
Huu ushamb sijui utaisha lini??
Vema hata Mwandishi angesema tu " baadhi ya wanachama wa Yanga" ndio wamefanya hilo tukio badala ya kuandika kama vile wanachama walio wengi ndio wamefanya hivyo.
 
Mleta mada nawe unatatizo kubwa. Mbona hiyo heading ni kubwa kuliko tendo? Ati Wanachama wa Yanga. Mimi mbona sikuwepo wala sikushirikishwa? Gazeti lenyewe moja tena lililetwa ofisini bure halaf ndio limechanwa chanwa likawashwa na kiberiti cha sigara kali. Nayo hiyo ni hoja kweli ya kuandika humu jf?
Hivi wanachama wote wa Yanga kama wangeenda Jangwani hali ingekuaje?
 

Wanachama wa Yanga wamecharuka na kufanya kitendo kinachoonyesha ni hasira kutokana na kuchana na kuchoma moto magazeti.
Wanachama hao wa Yanga, leo wamechoma moto magazeti ya Nipashena The Guardian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Wanachama hao wamefanya hivyo wakipinga Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusakamwa kw amakusudi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
“Hii sasa imetosha, huyu Mengi na magazeti yake anamsakama Manji kila anapoona Yanga inafanya vizuri. Mara tu baada ya Yanga kutinga robo fainali hatua ya Kombe la Shirikisho, basi vyombo vyake vimeanza kuandika kwamba anatakiwa sijui kuondolewa Coco Beach.
“Hakuna asiyejua Manji amestaafu Quality Group, sasa anamtaja wa nini. Au anataka ashindwe kufanya kazi za Yanga kwa utulivu.

“Watuache, kweli tutatangaza watu wa Yanga waachane na kununua bidhaa zake,” alisema Abuu Chehekaheka.
Pamoja naye, wanachama wengine kama Edward Matiku, Clement Michael na Hashimu Mtanza nao walimuunga mkono pamoja na wengine waliokuwa pale kabla ya kuanza kuchoma moto magazeti hayo wakionyesha kuwa na jazba.

Hata walipoulizwa sababu kuu za kuchoma magazeti hayo yanayomilikiwa na Mengi, hakuna aliyetaka kujibu huku wakionyesha kuwa na jazba.

 
Mambo mengine aibu sana hata kuyasimulia. Hawa ndio baadhi ya 'wadau' ambao mimi huwa nalia nao sana.

Wananunua ugomvi usiowahusu kwa karanga za kuonjeshwa.
 
Nilidhani wamewavamia wauza magazeti na kuyachoma,kumbe wameyanunua!!Hili zoezi likiwa endelevu tena nchi nzima,Mengi atatengeneza pesa sana.

Mimi nawasihi wana Yanga wote kila siku asubuhi wanunue kila mmoja nakala mojamoja za NIPASHE na Guardian halafu wazichome moto. Lazima huyu Mengi akione cha moto mwaka huu.....NB naomba manji atenge fungu maalumu kwa zoezi hili....
 
Mafisadi ni wajanja sana.
Wameshawanunua baadhi ya wanachama ili wahalalishe ufiasadi wao. Kama Cocobeach inamuhusu awajibike asijifiche nyuma ya Yanga wala CCM.
Na mwaka huu Magufuli akiamua kutenda haki sawa kwa wote wataikimbia hii nchi. Yanga ina tija gani kwa taifa kama itatumika kama kichaka cha mafisadi?
Club ni kwa ajili ya kuburudisha tu na sio kutumika kutuibia.

Kama kuna ukweli kwenye tuhuma hizo basi atumbuliwe.
Hii nchi tumebaki nyuma sana kwa mambo ya kipumbavu.

Mtu anatuhuma halafu anapanga watu wa kumpigia kelele .
Mara wengine wanatetewa kidini,wengine kikabila,wengine kikanda ,wengine kichama na kisiasa na sasa Wamekuja kisoka. Ajabu kabisa. Hao wanachama wananufaika nini endapo serikali itakua inahujumiwa na matajiri ili kufadhili vilabu?
Yani miundo mbinu ya Taifa iharibiwe ili kulinda mfadhili wa timu?
Je,siku akifa ina maana taifa letu ndio litaishia hapo?
Mkuu wala usipoteze muda na hao wavamizi na waharibifu wa makazi ya vyura pale Jangwani.
 
Mengi ni shabiki wa Yanga na mfanyabiashara kama Manji. Hakukuwa na haja ya kuihusisha timu(brand ya Yanga) na ugomvi kati ya wafanaybiashara hawa wawili maana ugomvi wao upo bayana na ni wa muda mrefu. Manji hatakuwepo milele Yanga, hivyo si vizuri kuwafanyia fujo,dharau na kejeli wadau wengine wa Yanga kwa sababu ya Manji. Pia Manji atambue kuwa hao wanaopigana vita kwa niaba yake, ipo siku watapigana dhidi yake maana hawana maslahi na timu, bali mtu binafsi.

Kukosa ueledi katika masuala ya soka, ndio chanzo cha kudorora kwa timu zetu kimataifa. Tukatae kuharibu brand ya Yanga kwa maslahi ya mtu binafsi. Pamoja na mafanikio tuliyoyapata chini ya Manji, Yanga ni kubwa kuliko yeye. Manji si Yanga, wala Yanga si Manji.
Uko sahihi mkuu..ila ukweli Manji keshawaweza mapoyoyo wengi pale Yanga..ila kuna siku atawaliza..trust me ipo hiyo siku.
 
Mashabiki wa Yanga Luninga kwa kweli ni mamburula... Tatukuru wakija pita hapo sijui watamficha Manji hapo... kwenye MAFURIKO...

Na viwanja vya hapo walipo wanatakiwa wavunje hilo Jengo sehemu hatarishi....

Hapo Udini na kupewa pewa pesa za kulinda mfuko wanaona Manji mtu wa Maana..

Ila Mengi ana kimavi na Mirangi ya Kijani na Njano hajui tu na sijui anaipenda kwa nini ana damu ya kunguni tuseme... CCM walijiapiza kutotizama ITV kwenye uchaguzi ilipendelea sana upinzani... japo kwa kumsingizia wakati habari zake zilikuwa zinabalance ujinga wa baadhi ya wanachama hawataki upinzani uoneshwe... ila Mengi aendelee na msimamo wake wa kutoagua story Kampuni yake ibaki kuwa Super Brand.. Ndio Maana haichuji... walizokuwa wanazipenda ndio zimekosa radha... huu Ubaguzi ubaguzi sio siasa zetu Haki sawa kwa Wote ndio Msingi wetu tuendelee....

Unachoma Gazeti kila limemtaja Mwizi aliyemo ndani mwako... so Anaiba ili wewe ule... Mbabu pu zenu
 
Back
Top Bottom