Wanachofanya AZAM TV kwenye mpira ni uhuni na utapeli, wadau amkeni

Siku azam wakilogwa copyright ya kuonyesha NBC premiere L. Ikaingia dstv au kwingine kokote,basi hapo ndiyo nafunga nao mkataba rasmi kulipia kifurushi.
Na ndio ligi ya Tanzania itakaporudi kule kule Timu ndogo kuziomba simba na Yanga nauli.
 
Kuna tofauti media ikitangaza inaonyesha MECHI za ligi Fulani..
Na media ikisema inaonyesha LIGI ya nchi Fulani..
Rudia kusoma

We nawe sio kila mwenye azam kachukua kwa ajili ya sport kuna watz wengi hata masuala ya mpira hawako nayo xx wataka chanel zote zionyeshe mpira tuh?
Mwingine atataka chanel nyingi za movie
Mwaingine ye ni mziki tuh...xo hao wote lazima ubalance chanel
 
Siku azam wakilogwa copyright ya kuonyesha NBC premiere L. Ikaingia dstv au kwingine kokote,basi hapo ndiyo nafunga nao mkataba rasmi kulipia kifurushi.
Subiri miaka 8 ijayo ndo ufanye huo uamnuzi kwani Azam na TFF ni Hadi 2030
 
Wabongo mnalalamika Sana aisee. Ile Ni biashara ya mtu, USIMPANGIE! ukiona wahuni simple tu, ingia dstv au startimes

Azam wamesaidia kwa mengi, na kwa kuwa hawawezi kumfurahisha kila mtu we potezea tu, achana nao eiza ingia hizo kampuni zingine au anzisha ya kwako mkuu uwe na channels Mia 9 kama unahisi ni rahisi
Hamna biashara pale matapeli
 
Wazee wa local content,ila very expensive na huu mgao wa umeme silipiii ng'oooooook,25 naenda kumpa mama yangu ale bata tuuuuu
Penda vya kwenu kijana vitu vyenu unaviita local
Watu weusi bado tunatawaliwa na ujinga kwa kuwatumikia watu weupe yaani utumwa mamboleo
 
Wakuu Azam tv hivi karibuni imeanza uhuni ambao lazima ukemewe!

Azam walijinasibu kuonyesha ligi ya ufaransa (Ligue 1) ligi ya ujerumani (bundesliga) ligi kuu ya Tanzania (NBC) na hivi karibuni wakasema na Ligue ya waarabu kwa kina Ronaldo ..
Ajabu Leo hii nimeona tena kesho wanaonyesha ligi kuu ya KENYA!

Uhuni/utapeli uko wapi?

Azam Wana channel tatu tu za michezo na Moja (zbc 2) Huwa wanaazima so tuseme jumla zipo 4..

Sasa uhuni unakuja siku za weekend ambapo ujerumani, ufaransa, Tanzania, na uarabuni na pengine huko Kenya Kuna mechi ambazo zipo ndani ya muda mmoja!

Basi hapo Azam wanaamua wao ni mechi Gani waonyeshe! Na ipi wasionyeshe!

Mbaya zaidi Kuna zile mechi 'kubwa' za siku utakuta hawaonyeshi kwa kuwa channels hazitoshi,,.

Nasema hivi
Huu ni uhuni na utapeli Azam, 25000 kwa mwezi ni kubwa sana punguzeni au ONGEZENI CHANNELS

Ili mkisema mnaonyesha ligi Fulani ni sisi watazamaji tuamue mechi ya kuangalia sio nyie mtuchagulie
********

MY TAKE
Azam watangaze kuwa wanaonyesha Badhi ya MECHI ZA LIGI FULANI
Wasiseme wanaonyesha LIGI YA NCHI Fulani..

Wakifanya hivi sitakuwa na kesi nao
Hivi kwanini TBC wasiwe na channel ya michezo tu, japo hata waoneshe ndondo cup, chandimu na umiseta?
Kuwategemea Azam pekee ndio tunaishia kupata tabu hizi.
 
Mie hawa azam kisimbuzi chao nina miaka 5, sijawahi kukutumia, nilipo hama nilikiwcha huko huko.
 
Leo game za Bundesliga hawaoneshi[emoji1787][emoji1787]
Hawa jamaa wababaishaji sana!
 
Isingekuwa NBC league hichi king'amuz chao ningeshapiga kiberiti, hakina cha maana wala quality ya picha, channels za HD ni 3 tu nyingine picha hazina tofauti na TBC
 
Dstv full shangwe hakuna uswahili uswahili....mambo buridan channels zote full HD
 
Hivi kwanini TBC wasiwe na channel ya michezo tu, japo hata waoneshe ndondo cup, chandimu na umiseta?
Kuwategemea Azam pekee ndio tunaishia kupata tabu hizi.
Ila kuanzisha channel kwa ajili ya Sports tuu sio jambo dogo, imagine kufanya content za sports tuu Wakati tayari Azam wanajulikana kuwa ndo kazi zao
 
Wakuu Azam tv hivi karibuni imeanza uhuni ambao lazima ukemewe!

Azam walijinasibu kuonyesha ligi ya ufaransa (Ligue 1) ligi ya ujerumani (bundesliga) ligi kuu ya Tanzania (NBC) na hivi karibuni wakasema na Ligue ya waarabu kwa kina Ronaldo ..
Ajabu Leo hii nimeona tena kesho wanaonyesha ligi kuu ya KENYA!

Uhuni/utapeli uko wapi?

Azam Wana channel tatu tu za michezo na Moja (zbc 2) Huwa wanaazima so tuseme jumla zipo 4..

Sasa uhuni unakuja siku za weekend ambapo ujerumani, ufaransa, Tanzania, na uarabuni na pengine huko Kenya Kuna mechi ambazo zipo ndani ya muda mmoja!

Basi hapo Azam wanaamua wao ni mechi Gani waonyeshe! Na ipi wasionyeshe!

Mbaya zaidi Kuna zile mechi 'kubwa' za siku utakuta hawaonyeshi kwa kuwa channels hazitoshi,,.

Nasema hivi
Huu ni uhuni na utapeli Azam, 25000 kwa mwezi ni kubwa sana punguzeni au ONGEZENI CHANNELS

Ili mkisema mnaonyesha ligi Fulani ni sisi watazamaji tuamue mechi ya kuangalia sio nyie mtuchagulie
********

MY TAKE
Azam watangaze kuwa wanaonyesha Badhi ya MECHI ZA LIGI FULANI
Wasiseme wanaonyesha LIGI YA NCHI Fulani..

Wakifanya hivi sitakuwa na kesi nao
Azam Media kuna shida kubwa ya viongozi wengi kukosa weledi na dira ya wapi wanataka taasisi hiyo kuelekea.

Na shida kubwa ni aina ya ajira zao kuwa za kijamaa na urafiki, na sio uzoefu na taaluma. Ndiyo maana haya yanatokea.

Viongozi wengi pale hawafukuziki hata wafanye makosa ya namna gani, kwa sababu labda wameletwa na Yusuf.

Niliwahi kuzungumza na Tido wakati akiwa pale, nikimuuliza kukosa kwao kukua, kwa maana ya kuongeza channels za michezo.

Alisema kuwa, amekosa timu sahihi ya kukuza taasisi, kwani wakati wote akitoa maelekezo/ mwongozo huwa kuna utekelezaji hafifu.

Fikiria, baada ya kustaafu Tido kwa sasa Kahemele ndiyo kiongozi Mkuu pale, ila yeye yuko kwenye nafasi hiyo kwa kuwa walikuwa naye kwenye timu ya Azam kabla kuanza TV.

Hadi sasa wana miaka kumi tangu walipoanza, ila bado wana channels saba au nane tu, nyingine zote siyo zao. Kuna shida pale.

Ova
 
Wabongo mnalalamika Sana aisee. Ile Ni biashara ya mtu, USIMPANGIE! ukiona wahuni simple tu, ingia dstv au startimes

Azam wamesaidia kwa mengi, na kwa kuwa hawawezi kumfurahisha kila mtu we potezea tu, achana nao eiza ingia hizo kampuni zingine au anzisha ya kwako mkuu uwe na channels Mia 9 kama unahisi ni rahisi
Jifunze kuwa mnunuzi wa bidhaa ni sehemu ya hiyo biashara, maoni na malalamiko yake ni sehemu ya kuboresha huduma.

Ova
 
Back
Top Bottom