Wanafunzi 3,000 Waliopata ujauzito na sababu mbalimbali warudi Shuleni. Benki ya Dunia yaahidi kuongeza misaada

Wanafunzi 3,000 Waliopata ujauzito na sababu mbalimbali warudi Shuleni. Benki ya Dunia yaahidi kuongeza misaada

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
IMG-20220711-WA0022(1).jpg

Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa kuamua kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye maeneo ya uzalishaji kikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi mambo ambayo yatachochea ukuaji wa kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Aliahidi kuwa Benki yake na washirika wake wengine watasaidia juhudi za Serikali za kufanikisha mapinduzi katika sekta hizo muhimu kwa kutoa fedha pamoja na ushauri wa kitaalam ili mpango huo wa kuendeleza kilimo, mifugo na uvuvi uwe na tija.

Bi. Kwakwa alisema kuwa changamoto ya UVIKO 19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine vimeibua changamoto kubwa ya uhaba wa mazao ya nafaka na kwamba Tanzania ikijipanga vizuri inaweza kuwa ghala la chakula na kuifanya ijitosheleze kwa chakula na kutoagiza chakula kutoka nje.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Serikali imeamua kuwekeza fedha kwenye maeneo ya uzalishaji akitolea mfano wa ongezeko la bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 200 hadi zaidi ya shilingi bilioni 900 ili kuiwezesha sekta hiyo kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuzalisha ajira kwa wananchi.

Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 2.8 katika miradi 11 ya kimkakati iliyowasilishwa katika Benki hiyo katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa uwekezaji huo utaisaidia nchi kupambana na umasikini pamoja na ukuaji jumuishi wa maendeleo ya watu na kuahidi kuwa fedha zinazopatikana kutoka katika Benki hiyo zinatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Nchemba, aliishukuru Benki hiyo kwa kuiidhinishia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango mpya wa utoaji mikopo na misaada wa IDA 20 ulioanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2022.

Aliiomba Benki hiyo kuharakisha utoaji wa fedha ili miradi iliyopangwa kutekelezwa kupitia mpango huo wa miaka mitatu iweze kutekelezwa na kwamba Serikali itashukuru endapo kiwango hicho cha fedha kitaongezwa ili miradi iliyopo hivi sasa inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani bilioni 4.9 iweze kukamilika kwa wakati.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipamgo, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamisi Shaaban, Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Rished Mohamed Bade na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
292857776_725787798646451_6071359685648899544_n.jpg

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bi Victoria Kwakwa Julai 11, 2022 ametembelea shule ya Sekondari Turiani Jijini Dar es Salaam ili kujionea maendeleo ya Programu ya SEQUIP ambayo sehemu ya utekelezaji wake ni mpango wa kuwarudisha shuleni watoto walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ili waweze kuendelea na masomo yao.

BENKI ya DUNIA (WB) imeahidi kuendelea kutoa msaada kwa Serikali ya Tanzania baada ya kushuhudia utekelezaji wa Mradi uliowarejesha zaidi ya watoto 3000 walioshindwa kuendelea na Masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo na kupata ujauzito.

Hayo yameelezwa leo Tarehe 11 Julai 2022 na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Victoria Kwakwa alipofanya ziara kwenye shule ya Sekondori ya Turiani Kinondoni jijini Dar es Salaam akiambatana na Profesa Adolf Mkenda Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo alikutana na wanafunzi waliorejeshwa shuleni.

Wanafunzi hao wanaosoma kupitia mfumo wa elimu mbadala walioshindwa na Masomo kwa sababu za kupata ujauzito.

Victoria amesema WB inaendelea kuipa nguvu Serikali ya Tanzania hususani Wizara ya Elimu "Tutaendela kuisaidia Wizara ya Elimu kwa jitihada zao za kufanya mageuzi kwenye elimu itakayoifanya Tanzania kuendelea zaidi".

Kwakwa ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku mbili amesema kuwa amefurahi kuona watoto wakiwa na tabasamu linaloashiria furaha "Nimeshudia watoto wakifurahia kurejeshwa shule "
292957642_374836674738644_1443461989161832928_n.jpg

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini, Bi Victoria Kwakwa amefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa kuwarudisha shule wanafunzi walioacha masomo kutokana na changamoto mbalimbali. Zaidi ya wanafunzi zaidi ya 3000 wamerejea shule kupitia mpango huo.

Amemsifu Rais Samia kwa jitihada zake za kuwarejesha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo "Katika shule hii tumeona maendeleo ya wazi ya Serikali ya Rais Samia katika kuimarisha sekta ya elimu hasaa kwenye Maendeleo ya Vijana wa Tanzania"

"Leo tumejionea Programu ya elimu mbadala kwa watoto wa kike na wakiume waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali wamepewa nafasi nyingine ili wapate elimu .
Ni Programu nzuri zaidi ya watoto 3000 wamerejea shuleni jambo ambalo limerejesha tabasamu kwa watoto hao" amesema Victoria

Waziri Profesa Mkenda akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa Kwakwa ametembelea darasa la wanafunzi waliorejeshwa shuleni kwa mfumo wa elimu mbadala ambayo ni sehemu ya mredi wa Maendeleo ya shule za Sekondori (SEDP) unaodhaminiwa na Benki ya Dunia.

Amesema kuwa Mradi huo unathamani ya Dola za kimarekana 500 Milioni unaolenga kuboresha elimu nchini.

Amesema kuwa Serikali imeamua kuwarejesha shuleni mabinti wasome ili kufufua ndoto zao za kielemu.

Amesema kuwa Serikali imewarejesha watoto 3333 walioshindwa kuendelea na masomo ambapo 900 wamerejea kwenye mfumo wa elimu ya kawaidi na waliobaki kwenye mfumo wa elimu mbadala ambapo watasoma kwa miaka miwili Kisha kufanya mitihani wa kuhitimu kidato cha nne.

Ameishukuru WB kwa kuisaidia Wizara hiyo "Benki ya Duania imetusaidia kwenye mambo mengi Wizara yetu imenifaika kwenye Mirada hii".

Amesema kuwa tayari Serikali imeshaanzisha Vituo kama hivyo 135 .
Amesema kuwa serikali hajaishia hapo inafanya juhudi za kuhakikisha wanafunzi hawakatizi masomo yao kwa sababu ya ujauzito.

"Tunahitaji kuwa na Vituo vingi zaidi tunafanya vitu viwili kwa wakati mmoja tunahimiza watoto wasome wasiingie kwenye mambo ya uzazi kwa wale ambao yashatokea hayo Rais ameagiza tusiwaache ndoto zao zikafa kwa hiyo huu ni utaratibu wa kuwarejesha waendelee na masomo yao" amesema Profesa Mkenda.

Salma Saidi mmoja wa wanafunzi waliorejea shuleni kwa mfumo wa elimu mbadala amemshukuru Rais Samia kwa kufufua upya ndoto zao.

"Nashukuru Rais Mama Samia kwa kuturejesha shuleni namuahidi hatutamuangusha".
 
Mikopo via IDA ni mizuri Sana maana Unapata msaada na mkopo wa masharti nafuu..

Hadi leo hii China anakopa kutumia Ida ,hii sio sawa kwa sababu wanabinya nafsi ya Nchi maskini.
 
Mikopo via IDA ni mizuri Sana maana Unapata msaada na mkopo wa masharti nafuu..

Hadi leo hii China anakopa kutumia Ida ,hii sio sawa kwa sababu wanabinya nafsi ya Nchi maskini.
Tatizo tunakopa ili kufanya nn? Ule mkopo wa kujenga ukumbi wa bunge haujalipwa hata mia, machinga complex haujalipwa, tumekopa kujenga matundu ya vyoo, hamna umasikini utaondoka kwa utaratibu huu
 
Tatizo tunakopa ili kufanya nn? Ule mkopo wa kujenga ukumbi wa bunge haujalipwa hata mia, machinga complex haujalipwa, tumekopa kujenga matundu ya vyoo, hamna umasikini utaondoka kwa utaratibu huu
Zamani sio sasa,mikopo ya Sasa iko wazi na Serikali imesema kwamba hatukopi kwa ajili ya kulipa salary au recurrent expenditure bali tunakopa kwa ajili ya miradi..

Sasa kuna watu mumekariri mnazani miradi ni madaraja na vitu kama hivyo ila ukikopa kwa ajili ya kuwezesha sekta wezeshi kama elimu unaona ni kama kupoteza pesa,hii dhana ya kijinga itoeni vichwani mwenu.
 
Honestly speaking mna kopa pesa kufanya minor things ambayo hamna trickle down effect, mmeleta sera za kijinga, kama kunyima mikopo walio soma privete schools, sasa watoto wote wamevamia Gvt schools,
 
Zamani sio sasa,mikopo ya Sasa iko wazi na Serikali imesema kwamba hatukopi kwa ajili ya kulipa salary au recurrent expenditure bali tunakopa kwa ajili ya miradi..

Sasa kuna watu mumekariri mnazani miradi ni madaraja na vitu kama hivyo ila ukikopa kwa ajili ya kuwezesha sekta wezeshi kama elimu unaona ni kama kupoteza pesa,hii dhana ya kijinga itoeni vichwani mwenu.
Zamani ipi ni nyie mko madarakani tangu uhuru,
 
Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa kuamua kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye maeneo ya uzalishaji kikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi mambo ambayo yatachochea ukuaji wa kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Aliahidi kuwa Benki yake na washirika wake wengine watasaidia juhudi za Serikali za kufanikisha mapinduzi katika sekta hizo muhimu kwa kutoa fedha pamoja na ushauri wa kitaalam ili mpango huo wa kuendeleza kilimo, mifugo na uvuvi uwe na tija.

Bi. Kwakwa alisema kuwa changamoto ya UVIKO 19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine vimeibua changamoto kubwa ya uhaba wa mazao ya nafaka na kwamba Tanzania ikijipanga vizuri inaweza kuwa ghala la chakula na kuifanya ijitosheleze kwa chakula na kutoagiza chakula kutoka nje.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Serikali imeamua kuwekeza fedha kwenye maeneo ya uzalishaji akitolea mfano wa ongezeko la bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 200 hadi zaidi ya shilingi bilioni 900 ili kuiwezesha sekta hiyo kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuzalisha ajira kwa wananchi.

Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 2.8 katika miradi 11 ya kimkakati iliyowasilishwa katika Benki hiyo katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa uwekezaji huo utaisaidia nchi kupambana na umasikini pamoja na ukuaji jumuishi wa maendeleo ya watu na kuahidi kuwa fedha zinazopatikana kutoka katika Benki hiyo zinatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Nchemba, aliishukuru Benki hiyo kwa kuiidhinishia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango mpya wa utoaji mikopo na misaada wa IDA 20 ulioanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2022.

Aliiomba Benki hiyo kuharakisha utoaji wa fedha ili miradi iliyopangwa kutekelezwa kupitia mpango huo wa miaka mitatu iweze kutekelezwa na kwamba Serikali itashukuru endapo kiwango hicho cha fedha kitaongezwa ili miradi iliyopo hivi sasa inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani bilioni 4.9 iweze kukamilika kwa wakati.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipamgo, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamisi Shaaban, Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Rished Mohamed Bade na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katika utawara wangu sisomeshi wamama!

Hadhira inapiga makofi👏🏽👏🏽👏🏽

Ama kweli maisha bila unafki hayaendi
 
Mumeshindwa kuendesha nchi mumeanza maneno ya kijinga
Tumeshindwaje? Walioshindwa wanaweza. fanya haya ? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220711-173642.png
    Screenshot_20220711-173642.png
    148.6 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220712-103211.png
    Screenshot_20220712-103211.png
    184.1 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220711-173620.png
    Screenshot_20220711-173620.png
    103.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220711-172628.png
    Screenshot_20220711-172628.png
    153 KB · Views: 8
  • Screenshot_20220711-172345.png
    Screenshot_20220711-172345.png
    157.8 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220711-140426.png
    Screenshot_20220711-140426.png
    185.5 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220711-140329.png
    Screenshot_20220711-140329.png
    172.8 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220711-115842.png
    Screenshot_20220711-115842.png
    150.7 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220710-193713.png
    Screenshot_20220710-193713.png
    158.1 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220710-193003.png
    Screenshot_20220710-193003.png
    195.9 KB · Views: 5
M

Miradi yote hiyo haiondoi umasikini wa mtu mmoja mmoja, inakuza Matumizi ya Serikali na kuongeza mzigo wa kodi kwa mlaji
Umaskini unaondoka kwa serikali kutofanya miradi?

Umaskini unaondoka kwa serikali kugawa pesa au?

Sasa kalisha buttocks zako kindezi usichangamkie fursa utaona utakavyopauka kwa umaskini,sio kazi ya serikali kukuondolea wewe umaskini bali kukuwekea mazingira rafiki ujiondolee umaskini ikiwemo hiyo miradi wezeshi.
 
Yaan nchi inachukua mikopo kwa ajiri ya vibint vilivyovua chupi kiholela?? hy bhaana
 
Back
Top Bottom