View attachment 2287882
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bi Victoria Kwakwa Julai 11, 2022 ametembelea shule ya Sekondari Turiani Jijini Dar es Salaam ili kujionea maendeleo ya Programu ya SEQUIP ambayo sehemu ya utekelezaji wake ni mpango wa kuwarudisha shuleni watoto walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ili waweze kuendelea na masomo yao.
BENKI ya DUNIA (WB) imeahidi kuendelea kutoa msaada kwa Serikali ya Tanzania baada ya kushuhudia utekelezaji wa Mradi uliowarejesha zaidi ya watoto 3000 walioshindwa kuendelea na Masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo na kupata ujauzito.
Hayo yameelezwa leo Tarehe 11 Julai 2022 na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Victoria Kwakwa alipofanya ziara kwenye shule ya Sekondori ya Turiani Kinondoni jijini Dar es Salaam akiambatana na Profesa Adolf Mkenda Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo alikutana na wanafunzi waliorejeshwa shuleni.
Wanafunzi hao wanaosoma kupitia mfumo wa elimu mbadala walioshindwa na Masomo kwa sababu za kupata ujauzito.
Victoria amesema WB inaendelea kuipa nguvu Serikali ya Tanzania hususani Wizara ya Elimu "Tutaendela kuisaidia Wizara ya Elimu kwa jitihada zao za kufanya mageuzi kwenye elimu itakayoifanya Tanzania kuendelea zaidi".
Kwakwa ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku mbili amesema kuwa amefurahi kuona watoto wakiwa na tabasamu linaloashiria furaha "Nimeshudia watoto wakifurahia kurejeshwa shule "
View attachment 2287883
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini, Bi Victoria Kwakwa amefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa kuwarudisha shule wanafunzi walioacha masomo kutokana na changamoto mbalimbali. Zaidi ya wanafunzi zaidi ya 3000 wamerejea shule kupitia mpango huo.
Amemsifu Rais Samia kwa jitihada zake za kuwarejesha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo "Katika shule hii tumeona maendeleo ya wazi ya Serikali ya Rais Samia katika kuimarisha sekta ya elimu hasaa kwenye Maendeleo ya Vijana wa Tanzania"
"Leo tumejionea Programu ya elimu mbadala kwa watoto wa kike na wakiume waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali wamepewa nafasi nyingine ili wapate elimu .
Ni Programu nzuri zaidi ya watoto 3000 wamerejea shuleni jambo ambalo limerejesha tabasamu kwa watoto hao" amesema Victoria
Waziri Profesa Mkenda akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa Kwakwa ametembelea darasa la wanafunzi waliorejeshwa shuleni kwa mfumo wa elimu mbadala ambayo ni sehemu ya mredi wa Maendeleo ya shule za Sekondori (SEDP) unaodhaminiwa na Benki ya Dunia.
Amesema kuwa Mradi huo unathamani ya Dola za kimarekana 500 Milioni unaolenga kuboresha elimu nchini.
Amesema kuwa Serikali imeamua kuwarejesha shuleni mabinti wasome ili kufufua ndoto zao za kielemu.
Amesema kuwa Serikali imewarejesha watoto 3333 walioshindwa kuendelea na masomo ambapo 900 wamerejea kwenye mfumo wa elimu ya kawaidi na waliobaki kwenye mfumo wa elimu mbadala ambapo watasoma kwa miaka miwili Kisha kufanya mitihani wa kuhitimu kidato cha nne.
Ameishukuru WB kwa kuisaidia Wizara hiyo "Benki ya Duania imetusaidia kwenye mambo mengi Wizara yetu imenifaika kwenye Mirada hii".
Amesema kuwa tayari Serikali imeshaanzisha Vituo kama hivyo 135 .
Amesema kuwa serikali hajaishia hapo inafanya juhudi za kuhakikisha wanafunzi hawakatizi masomo yao kwa sababu ya ujauzito.
"Tunahitaji kuwa na Vituo vingi zaidi tunafanya vitu viwili kwa wakati mmoja tunahimiza watoto wasome wasiingie kwenye mambo ya uzazi kwa wale ambao yashatokea hayo Rais ameagiza tusiwaache ndoto zao zikafa kwa hiyo huu ni utaratibu wa kuwarejesha waendelee na masomo yao" amesema Profesa Mkenda.
Salma Saidi mmoja wa wanafunzi waliorejea shuleni kwa mfumo wa elimu mbadala amemshukuru Rais Samia kwa kufufua upya ndoto zao.
"Nashukuru Rais Mama Samia kwa kuturejesha shuleni namuahidi hatutamuangusha".