Mzigua90
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 38,342
- 88,625
Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe". Mama akamwambia "we mtoto nina mtoto kama wewe nyumbani usinijibu vibaya". Mwanafunzi akamjibu "mama kama mtoto yuko kwako ungekua na mtoto kama mimi ungemleta kwenye garia saa hizi mbona hayupo kwanza achana na mimi na stress zako za kutolipwa mshahara".
Haki nilijisikia vibaya yule binti kumjibu vile mama wa watu. Sawa sio jambo zuri kumsimamisha mwanafunzi ili mtu mzima akae lakini yule binti ana mdomo mchafu sanaa. Kwa style hii hawa wanafunzi wa Dar wataendelea kufeli kwa sababu hawana adabu kwa mkubwa wala mdogo. Nimewazia walimu wake atakua anawajibu dharau kiasi gani wakiwa wanamgombeza.