Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anamwambia mtu mzima kama mama yake etia anatafuta kik. Mpaka yule mama kaacha kuongea mwamafunzi anachamba tuNadhani chanzo hapo ni sisi wazazi tunaowalea. Sababu angelelewa vyema na Mzazi au Mlezi nyumbani basi hadi hapo angekuwa na heshima.
Hili ni somo kwa wazazi na walezi kwamba tulee watoto katika mstari ulionyooka kuanzia chini.
Japo kanikera sana huyo mtoto.
Ni kama laanaZero wanakosaje hawana adabu.
Alivyoshuka ndo mama mwingine akaanza kumsema ila alivyokuepo wote tulipiga kimya maana kama aliweza mjibu yule mama sisi ni kina nani angetujibu tuNdo dar ilivyo, mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio,ingekua mkoani uyo mtoto ungekuta kashacharazwa bakora za kutosha
Hakukua na mtu wa kumzaba makofi mawili matatu hiviSana yani halafu haoni aibu anaongea kwa sauti watu wote tunamsikia. Badala angejibu chini chini ila anavyojiamini hakujali tutamchukuliaje ye anampa maneno tu mama wa watu
Ingekua kijijini angekula fimbo. Sema yule anaonekana hata kwao anawasumbua. Unapata wapi ujasiri wa kumsema vibaya mama mtu mzima tena bila woga kwenye daladala ilojaa jamani.Mtoto sio wa jamii tena bali ni wa baba na mama yake tu
Watatuvua sana nguo tujiandae kisaikolojia
Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe". Mama akamwambia "we mtoto nina mtoto kama wewe nyumbani usinijibu vibaya". Mwanafunzi akamjibu "mama kama mtoto yuko kwako ungekua na mtoto kama mimi ungemleta kwenye garia saa hizi mbona hayupo kwanza achana na mimi na stress zako za kutolipwa mshahara".
Haki nilijisikia vibaya yule binti kumjibu vile mama wa watu. Sawa sio jambo zuri kumsimamisha mwanafunzi ili mtu mzima akae lakini yule binti ana mdomo mchafu sanaa. Kwa style hii hawa wanafunzi wa Dar wataendelea kufeli kwa sababu hawana adabu kwa mkubwa wala mdogo. Nimewazia walimu wake atakua anawajibu dharau kiasi gani wakiwa wanamgombeza.
Ishu sio kumpisha kiti mtu mzima. Hata mimi sipendagi hilo jambo la kumwambia mwanafunzi ampishe siti mkubwa. Ila yale majibu yake hakua na stahaKwani gari zilikuw zimeisha mpak mtu mzima upande gari lililo jaa hapo utakuwa umeamua kufanya mazoez
Mungu anisamehe ila yule anaonekana anaenda shule kusindikiza wenzie tu. Form four yake naona zero kabisaNdio hapo sasa. Sababu mtoto kama hana adabu kiasi hicho sidhani kama anaweza muheshimu mwalimu wake na kutokumuheshimu ndio mwanzo wa kufanya vibaya darasani sababu hakuna kitakachoingia.
Sababu katika kusoma nidhamu nayo ni muhimu.
Ila ndugu yangu nimecheka kama mazuri ujue.Anamwambia mtu mzima kama mama yake etia anatafuta kik. Mpaka yule mama kaacha kuongea mwamafunzi anachamba tu
Angemdanganya hata najisikia vibaya naumwa. Ni bora kudangaanya kuliko yale majibu aiseeMkuu kinachozungumziwa ni yale majibu machafu.
Kwani angeamua kulaza kichwa kwenye siti ya mbele yake kama wanavyofanyaga au kukaa kimya na kutokujibu huu uzi ungekuwepo?