Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Leo kwenye daladala kuna mama alimwambia mwanafunzi ampishe mzee akae. Yule mwanafunzi badala ya kujibu kistaarabu labda mama nimechoka au nnitalipa nauli ya mtu mzima ila alichokifanya ni kujibishana na yule mama. Akaanza kumwambia simpishi mtu angetaka angewahi. Mama kujibiwa vile akapata moto. Akamwambia nyie watoto wa siku hizi hamna adabu mzee kasimama wewe umekaa halafu unajibu vibaya. Mwanafunzi akamwambia mama "usitafutie kik kwangu kama una stress mshahara hujatoka achana na mimi." "Kwanza nakushangaa unavyoniambia nimpishe si ungempisha wewe". Mama akamwambia "we mtoto nina mtoto kama wewe nyumbani usinijibu vibaya". Mwanafunzi akamjibu "mama kama mtoto yuko kwako ungekua na mtoto kama mimi ungemleta kwenye garia saa hizi mbona hayupo kwanza achana na mimi na stress zako za kutolipwa mshahara".

Haki nilijisikia vibaya yule binti kumjibu vile mama wa watu. Sawa sio jambo zuri kumsimamisha mwanafunzi ili mtu mzima akae lakini yule binti ana mdomo mchafu sanaa. Kwa style hii hawa wanafunzi wa Dar wataendelea kufeli kwa sababu hawana adabu kwa mkubwa wala mdogo. Nimewazia walimu wake atakua anawajibu dharau kiasi gani wakiwa wanamgombeza.
 
Watoto wa siku hizi ni bure kabisa ukichangia na ujuaji mwingi ni hatari sana.

Wanajiona wakubwa sababu mambo wanayoyafanya wakubwa nao wanafanya.

Na kikubwa zaidi tabia zozote alizonazo mtoto zinachangiwa kwa asilimia kubwa na malezi aliyopewa.

Tuzidi kuwaombea tu maana wanahitaji neema ya Mungu kujirekebisha makosa yao.
 
imeniumiza sana
 
Nadhani chanzo hapo ni sisi wazazi tunaowalea. Sababu angelelewa vyema na Mzazi au Mlezi nyumbani basi hadi hapo angekuwa na heshima.

Hili ni somo kwa wazazi na walezi kwamba tulee watoto katika mstari ulionyooka kuanzia chini.

Japo kanikera sana huyo mtoto.
 
Yani kama yule lazima ameshakua na mambo ya wanaume ndo maana ana confidence kiasi kile.
 
Halafu wakifeli walimu wanawajibishwa..kwa staili hii walimu nawahurumia mtapata tabu sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…