Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Mgejibu tu na nyie mngejibiwa mpaka mngelia
Weeee. Mimi najibishanaga na maneno ya kukuumiza. Yani angejisikia vibaya yule mtoto. Nilishamjibu mtu halafu alinikosea sana sana sana. Wakati yeye anapayuka mimi namjibu chini kwa chini ila yale yanayouma. Mwisho wa siku akalia yeye wakati mimi ndo alinikosea na wala sikutoa chozi
 
Huyo mtoto kanisikitisha sana na hana adabu. Lakini na sie tuache kutumia umri wetu mkubwa kuingia kwenye daladala limejaa tukategemea kupishwa, ukijisikia unataka kukaa subiri kali jingine achana na hilo lililojaa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kama nakuona
 
Mzigua90 hapo ni unajisemea wewe. Kila aliyewahi kua mwanafunzi ameshaonja usumbufu.

Nikisema niulize ni wangapi wamewahi kulipiwa nauli ili wasisimame tunaweza kuwapata wachache sana sawasawa na ningeuliza nani aliwahi kutetewa alipopigana na konda.

Mara zote lawama ni kwa mwanafunzi.
Tunavuna tulichopanda.

Binafsi mpaka leo nipo selective sana katika kusimama ili mtu akae naweza nikamuacha mwanafunzi akae kuliko kumpisha mtu wa miaka 60 kwenye siti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…