Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

Mada muhimu kweli. Na mimi nipo katika wakati huo huo mgumu, nimemaliza form four mwaka jana na nimefaulu vizuri sana ila hapa ninawaza na kuwazua sana niende advance au chuo..??
Umefaulu masomo yapi?
 
Fuatilia kwa ukaribu sana soko la ajira hapa kwetu.

Elimuni huko dip wana ajiriwa kwa wingi ukilinganisha na dig,hii hutokana na viwango vya mishahara kupishana.

Wakati mwingine huko 5&6 km mtu analenga kuwa Mwl ni kupoteza muda,ajira zenyewe ni za kunyakuana.
 
Ushauri mzuri sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Nenda unakotaka kuelekea kwa upande wa diploma. Hakikisha unafaulu. Achana na Advance.
yaani mwenyewe nawaza sana kwenda advance haiji akilini kabisa japo sijui watu watanichukuliaje ukilinganisha na walimu wa shule yangu
 
Huwezi kutengeneza wahitimu mahiri wa degree bila vijana kwenda A-level......ni muhimu vipanga wapitie chekeche la A-level ili wajipime ukipanga wao. Wale wenye uelewa wa kawaida ni sahihi kabisa kwenda diploma maana ukijipendekeza A-level ni rahisi sana kutaga mayai.​
 
Ni sahihi lakini kwa elimu yetu haina ukombozi zaidi ya kila mtu kuwaza buyu la asali.
Kwa mziki wa advance, Ni heri kutulizana diploma.
 
ni kwenda tu kukuza ubongo wa mtu ila practically haisaiidii sana maana they are more in theories than practices
 
Kwenda Chuo badala ya Advanced ni kitu kizuri sana! Mtu anakuwa amejitambua na anatambua career yake mapema na hivyo hataki kupoteza muda tena.

Tena ingewezekana na hiyo elimu ya sekondari kufanyiwa marekebisho, wanafunzi wangepata kuanza kupalilia career zao mapema baada ya kumaliza elimu ya msingi.

Elimu yenye maana hapa kati ya msingi, sekondari na advance ni elimu ya msingi.

Mtu akimaliza elimu ya msingi anaondoka na ujuzi mkubwa sana katika maisha ambao ni kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Sasa kwa elimu ya Tanzania, ebu jifikirie mwenyewe, mtu akimaliza elimu ya sekondari, miaka 4, ameondoka na ujuzi gani? Jibu ni HAKUNA. Tena akaenda advance miaka mingine 2, anatoka na ujuzi gani? Endelea kujifikiria kama elimu ya Advance inamwandaa mwanafunzi kufanya nini? Mtu anaweza kusema kusema inamwandaa kwenda chuo kikuu; na yule ambaye hakwenda chuo kikuu anabakia na nini? Nothing!

Ni wakati muafaka sasa Tanzania tukabadilisha mfumo wetu wa elimu uendane na matakwa ya jamii kuliko kung’ang’ania migumo isiyokuwa na tija kwenye elimu yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…