Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

Mimi binafsi nilikuwa napenda sana kwenda advance then 2016 nilifanikiwa kujiunga advance mchepuo wa PGM ila kwa bahati mbaya tokeo halikuwa zuri hvyo nikashindwa kuendelea na degree... sikuwahi penda kusoma diploma ila kutokana na matokeo yangu ilinilazimu tena kurudi Diploma 2018..nilifanikiwa kupata chuo cha madini(MRI)Dodoma kozi ya Geology and Mineral Exploration..

Namshukuru Mungu nilimaliza vizuri mwaka 2021..ila mpaka muda huu sijafanikiwa kupata kazi ya kudumu ..ila nimepanga kuendelea na degree mwaka huu mwezi November kama nitakuwa sijapata kazi permanent.


Kama kuna dogo yupo olevel ni bora aunge diploma kwanza uhakika wa kufaulu kuendelea na degree ni mkubwa sana kulinganisha na advance pili unakuwa na uwanja mpana kwenye soko la ajira ..mfano mm mwenyewe now nikitaka kwenda kusoma degree naweza badilisha kozi hvyo nakuwa na uwezo wa kuomba kazi mbili tofauti kwa kutumia cheti changu cha diploma na degree.


Nawasilisha ..mwenye connection ya mambo ya geology tushirikishane .
 
Haha A level physics ilichonifanya najuta kupitia njia hii asee E ya physo ni fedheha kwelikweli 🚶🚶
 
Mayai nimeyataga sana kwenye mitihani ya ndani 😂😂😂 ila nikachomoa fresh necta
 
ndio ni pcm
Hakikisha unaionea chemistry na pure ndo masomo pekee yatakayo kukomboa mkuuu kama upo dar zuka hapo mchikichini kwa mudy physics

Muda ni sasa mi nilipoteza muda sana ningejuaga ningepiga 1 ya maana A level sema ndo ivyo tena nikaishia 2

Ila chemistry na math zimenisaidia sana

Mkuuu
 
Yaani mkuu ungejua kuwa na hata moja ya sababu zinazonifanya nifikilie kutokwenda advance ni hilo la kusoma twit muda huu
 
Yaani mkuu ungejua kuwa na hata moja ya sababu zinazonifanya nifikilie kutokwenda advance ni hilo la kusoma twit muda huu
Haha ni ngumu sana ila ndo hivyo tena utafanyaje

Mi stress na depression zilinikunguta sana huko A level kuliko saivi imagine

Tu mwaka 2021 nimepiga test zote division 0 nusu nifukuzwe shule daaah







Advance ni hell of a journey ☺️😅😅
 
Aya ya mwisho umedanganya. Aliyepitia advance ndiye mwenye nafasi ya kusoma kozi nyingi zinazotolewa na vyuo vikuu ngazi ya degree. Mfano PCM anasoma kozi zote za engineering na baadhi ya kozi za art (Accounting, Economics, e.t.c). Plus Deploma zote. Mtu mwenye uwezo hawezi kufeli advance. Mara nyingi wanaopitia diploma huwa wanaona uwezo wao hauwezi pambana na masomo ya advance. Kweli kama uwezo wako ni mdogo usipitie advance. Kingine kusoma diploma ni gharama kuliko kusoma advance. Kama huna mtaji wa kusoma diploma nenda advance. Ukipitia advance kuingia chuo kikuu ni rahisi zaidi.

Na vyuo vikuu vinapenda kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi waliopitia advance kuliko diploma (Hii inamaana ya kwamba wanafunzi wa diploma hawathaminiwi na vyuo vikuu kama wanavyo thaminiwa wanaotokea advance). Na wanafunzi wanaotokea advance ndio wanaoongoza kufanya vizuri vyuo vikuu kuliko diploma. Diploma masihara mengi na wengi huwa wanaishia kudisco au kupata supp.
 
Mimi nikienda advance nikawa na moyo na bidii angalau ya kusoma nitafaulu vizuri tu maana hata O level nimepata point nzuri tu lakini moyo huo sina na lazima kule mambo yatakuwa mengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…