Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

Tangazo la ajira la Muda Mambo ya Afya..unaambiwa Nurse awe Enrolled cheti cha miaka miwili ya Uuguzi na Ukunga.

Tuendelee kusoma Advance mdogo mdogo.
 
Si kweli, wapo Professors kadhaa ndani ya nchi yetu hawakupita A-level na wameweza kufanya vizuri sanaaa pengine kuzidi hata wale waliopita A-level. Mmoja namfahamu alishawahi kuwa waziri ndani ya nchi yetu na ni mtu mashuhuri tuu. Ameiheshimisha nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo na yupo Professor mmoja yeye alianzia certificate kabisa, ila wahitimu wa enzi hizo walikuwa competent hasa.......siku hizi elimu imekuwa kama bora liende na hii ni kutokana na serikali kutelekeza elimu ya umma na wao kuanza kusomesha watoto wao private.

Nyerere angefanya kama wanavyofanya sasa hivi sidhani kama wangefika hapo walipo maana wengi walitokea familia zenye umaskini wa kutupa lakini Nyerere aliwasomesha bure elimu ya umma hadi wamepata hadhi hizo walizo nazo sasa.

Wengine ndo hao walikuwa wachunga mbuzi kijijini akina madelu ila sasa kwa kuwa wanasomesha watoto wao Feza schools hawaoni umuhimu wa kuifanya elimu ya umma kuwa bora ili watoto wa wanyonge kama walivyokuwa wao enzi hizo nao watimize ndoto zao kupitia elimu. Pesa ambayo ingeboresha hali ya elimu yakiwemo maslahi bora ya walimu ndo inayolambwa asali na kupimwa kwenye urefu wa kamba, na huenda ndo zinazoagiza hayo mabasi mia mbili yanayosemwa.​
 
Mtoa mada anaonekana kuibeza Sana diploma.. Ni wazi kuwa Advance ni njia fupi kufika degree Ila Diploma ni njia rahisi Sana kujua career Yako, Kama mtu yupo diploma na akimaliza diploma na aliyemaliza Advance ni watu wawili TOFAUTI..
Advance inaweza kupoteza kabisa ndoto zako sababu unasoma vitu ambavyo Sio specialized na utakapo feli ndio pale utashindwa kurud nyuma na kuamua kuingia kwenye coz yyt ilimrad uwe chuo kikuu..

Shida kubwa iliyopo diploma ni kuwa na uhuru kwa wanafunzi wakiwa katika umri mdg ambao unaweza usizalishe matunda halisi ya diploma
 
Nadhani serikali yetu ndio ilianzisha huu mtazamo wa kuona advance ni Bora baada ya kuwapeleka huko wenye ufaulu mkubwa na wenye ufaulu mdogo kwenda chuo Cha kati...

Diploma ni mahali ambapo mtu anasoma fani husika na anakutana na watu wengi wenye ujuzi ambapo anapata room ya kujifunza vitu vingi ambayo vina mpa ajira au...

Mfano mzuri ni nchi zingine Kama Kenya hawana hizi advanced secondary
 
Wapo na yupo Professor mmoja yeye alianzia certificate kabisa, ila wahitimu wa enzi hizo walikuwa competent hasa.......siku hizi elimu imekuwa kama bora liende na hii ni kutokana na serikali kutelekeza elimu ya umma na wao kuanza kusomesha watoto wao private.

Nyerere angefanya kama wanavyofanya sasa hivi sidhani kama wangefika hapo walipo maana wengi walitokea familia zenye umaskini wa kutupa lakini Nyerere aliwasomesha bure elimu ya umma hadi wamepata hadhi hizo walizo nazo sasa.

Wengine ndo hao walikuwa wachunga mbuzi kijijini akina madelu ila sasa kwa kuwa wanasomesha watoto wao Feza schools hawaoni umuhimu wa kuifanya elimu ya umma kuwa bora ili watoto wa wanyonge kama walivyokuwa wao enzi hizo nao watimize ndoto zao kupitia elimu. Pesa ambayo ingeboresha hali ya elimu yakiwemo maslahi bora ya walimu ndo inayolambwa asali na kupimwa kwenye urefu wa kamba, na huenda ndo zinazoagiza hayo mabasi mia mbili yanayosemwa.​
Ni kweli mkuu, makali ya technical schools yameisha kabisaaaa. Kuna mtu mzima mmoja aliwahi niambia miaka ya nyerere waliokuwa wanapelekwa technical schools ni wale walifaulu vizuri sanaaaa(yaani ile cream hasa ndo wanapelekwa huko Musoma Technical, Moshi Technical n.k) lakini kaangalie hali ilivyo sasa kwenye hizi shule za technical utalia machozi. Hii nchi ni kama ina laana vile Mungu atusaidie..ukisoma historia ya baadhi ya vyuo vikuu kwenye nchi za wenzetu unaambiwa nyingine zilikuwa just a school lakini leo hii ni chuo kikuu chenye heshima yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binafsi nilivyomaliza form 4 mwaka 2008 nilifail nilibahatika kupata credit mbili yaani C mbili nikakosa kwenda advance.nikakata tamaa kabisa ya kusoma.ikizingatiwa nilimaliza form 4 na umri mdogo na hata kiumbo nilikuwa mdogo pia.wakati nimekata tamaa kumbe mzee wangu hakunikatia tamaa alifight kunichkulia form jitegemee za kurisit binafsi nilichukia neno 'kulisit' ila nikawa sina jinsi..nikajiunga pale jkt mgulani enzi za mkisi..nikafanya pepa nikafanikiwa kupata hizo credit ila moyo wangu uligoma kusoma advance kwa kweli..nilijiona nitafeli tena na kumuaibisha mzee wangu.wakati tunapigapiga story na wenzangu wakasema wao wanaenda chuo kusoma cerficate japo wamefaulu vzr tu kama mimi.na mimi nikaona hii ni fursa sasa nikapambane huko.nikapaleka wazo nyumbani Mzee aliwaka sana hataki niende chuo anasema mimi bado mdogo pia nakimbilia wapi wakati nina sifa zote za kusoma advance??!akaenda mbali akasema nichague shulee yoyote nitakayo nikasome...mimi nilimgomea..mzee kuona nimegoma akaenda kunitafutia shule mwenyewe hahaha akaja na form nyumbani ..nakumbuka ile shule iliitwa happyskillful ipo tabata segerea na ada walikuwa wanalipa milion kadhaaa.mzee akajua nitaipenda ila niligomaa.mzee alichukia sana.home naishi kama digidigi.ila mwisho wa siku alikubali niende chuo tu.nashukuru nilimaliza miaka ya 3 ordinary diploma salama na nikafanikiwa kujiunga na chuo kikuu.wale wenzangu wengi walioenda A level ilikula kwao..

kupitia changamoto yangu nimejifunza kitu,kwamba wazazi wengi hawana uelewa na hivi vyuo wanaona mtoto wao kuanza na cerficate ni kama kilaza vilee. pia wazazi wawe wanawasikiliza watoto wao wanataka nini.
big up kwa mzee kwa kunipigania japo nilikuwa mkorofi...wewe ni baba bora
 
Utafiti wa Wizara ya elimu unaonesha kwamba kumekuwa na Wimbi kubwa la Wanafunzi Kukacha Kidato Cha 5 na 6 badala yake Kujiunga Vyuo Vya Elimu vya kati ngazi ya Diploma.

Kwani Kuna nini huko Advance na huku Diploma Kuna nini wanakimbilia?

Je inaweka kuwa wanaona Elimu ya Kidato cha 5 na 6 haiwasaidii mtaani kulinganisha na Elimu ya ngazi ya Diploma?

Je, pengine ukijiunga A level unaenda Bachelor na Sokoni Bachelor haiziki kama Diploma?

Shida nini Wanafunzi mnakimbia Ugumu au?

View attachment 2568366
Hakuna ugumu wowote ni kupoteza muda tu na resources haina maana yoyote unaenda kusoma huko unaenda chuo kikuu UNAMALIZIA hakuna Ajira Mahala popote
 
Huo ndio umri mzuri wa kuanza kujenga profession yake. Tena angetakiwa akiwa na 18 ameshakuwa Technician wa Electronics au Laboratory afanye vitu vya maana! Siyo 18, hana analolijua zaidi ya kukariri majibu ya mitihani ya advance
Uko sahihi kabsaa, tatizo linakuja kwenye kuweza kuwathibiti hao watoto, waliowengi uharibikia hapohapo, serikali ilipobadirisha umri wa kuanza shule haikubadiri masharti/kanuni za mwanachuo anapokuwa chuoni, kwahiyo wamekuwa wakiwaachia kama watu wazima kumbe ni watoto.
 
Odinary diploma/ FTC inatengeneza watendaji wa vitendo wazur hasa fani za sayansi na engineering. Kwa sabb wahitimu wanakuwa competent kwa kuwa kule unaelewa fani yao kwa vitendo. Engineer aliyepitia udsm direct kutoka advance level anajua ledership na design tu ila njoo site sasa. Akutane na Fundi mchundo aliyetoka must/dit/arusha tech atakachomshinda ni design tu ila kuhusu kujua kaz sidhani atamfikia hata Robo. Nimekutana na graduate wengi waliotoka direct from chuo kikuu ni weupe mno katika utendaji wa vitendo
Hizi hoja ni za walioshindwa msuli wa PCM/PGM.
Mnapenda sana kujifarijii, lol
 
Mada muhimu kweli. Na mimi nipo katika wakati huo huo mgumu, nimemaliza form four mwaka jana na nimefaulu vizuri sana ila hapa ninawaza na kuwazua sana niende advance au chuo..??
Ufaulu wako ukojeee??
 
Huwezi kutengeneza wahitimu mahiri wa degree bila vijana kwenda A-level......ni muhimu vipanga wapitie chekeche la A-level ili wajipime ukipanga wao. Wale wenye uelewa wa kawaida ni sahihi kabisa kwenda diploma maana ukijipendekeza A-level ni rahisi sana kutaga mayai.​
Ongezaaa sautiiii.

Advance ina heshima na rahaa yake bhana.

Sijutii kupitaa f5 &6
 
Back
Top Bottom