A
Anonymous
Guest
Hoja ya awali ~ Law School of Tanzania ilitangaza kukamata wachache kwa udanganyifu wa mitihani, why wanafunzi wote turudie mitihani?
Sababu ilidaiwa kuwa mtihani ulivuja na kwamba kulikuwa na michezo ya watu kupeana majibu sababu Wanafunzi wameingia na simu, sasa umeanzishwa utaratibu mpya.
Utaratibu huo wa kufanya ukaguzi wa electric device kwakila anayeingia kwenye chumba chamtihani, nadhani hili ni wazo zuri na utaratibu kama huo ulipaswa kutumika tangu zamani lakini uzembe wao ndiyo umewaingiza wanafunzi wote kwenye shida ya kurudia mitihani.
Actually utaratibu huu ulitakuwa kuwa hivi siku zote ila tu walikuwa wanachukulia poa, maana sidhani hata zile kamera zilizopo kwenye majengo ya darasa kama zinafanya kazi, kama zinafanya kazi wangekuwa wanazitumia hizo pia kubaini wanaofanya udanganyifu.