Wasiwasi umetanda katika baadhi ya Vyuo Vikuu nchini Marekani huku vingine vikitoa tahadhari kwa Wanafunzi wa Kimataifa kurudi vyuoni kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo Donald Trump.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN, Vyuo hivyo vina wasiwasi wa kuwepo kwa marufuku ya safari (travel ban) kama iliyotokea Serikali ya Trump ilipoingia Madarakani mwaka 2017.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa wanaoweza kuathirika ni pamoja na raia wa nchi zilizolengwa mara ya kwanza ikiwemo Kyrgyzstan, Nigeria, Myanmar, Sudan, Tanzania, Iran, Libya, Korea Kaskazini, Syria, Venezuela, Yemen na Somalia.
Nchi zingine zinazohisiwa kuongezeka kwenye orodha hiyo ni China na India.
Ikumbukwe kuwa Trump ameahidi kuja na sera kali za Uhamiaji mara baada ya kurudi Ikulu ya White House.