Wanafunzi Shule ya Msingi Namalombe wasomea chini ya mkorosho

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa, kutokana na shule hiyo kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

site%203.jpg

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema wanafunzi wa darasa la saba, darasa la kwanza na darasa awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili,la tatu,la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo kimoja cha nyasi walimu na wanafunzi.

site%205.jpg

Darasa linalotumika na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Hayo yamebainika baada ya ziara ya Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara Hamis Dambaya ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu,ofisi na madarasa mengine huku yeye akihaidi atawapelekea madarasa matatu kutoka ofisi ya TAMISEMI.

CHANZO: ITV
 
Uza ndege hizo jenga shule hizo watoto watakuja kununua ndege kuliko wakikosa Elimu watakuja kuziuza scraper hizo...maana mnadhani wachache wanaopata Elimu bora wataendesha Nchi kwa kurithishana.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Tangu 2014 mpka 2021 darasa moja is it seriously 😂😂😂huu uchumi wa kati na mashaka tumepigwa kanyungwi🥴🥴
 
Jiwe invest elimu kwenye vichwa vya raia wako
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa
Tupia picha ya huo mkorosho basi..

Hata hivo tupo uchumi wa kati.

Mi-5 tena🙄
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa, kutokana na shule hiyo kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

site%203.jpg

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema wanafunzi wa darasa la saba, darasa la kwanza na darasa awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili,la tatu,la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo kimoja cha nyasi walimu na wanafunzi.

site%205.jpg

Darasa linalotumika na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Hayo yamebainika baada ya ziara ya Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara Hamis Dambaya ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu,ofisi na madarasa mengine huku yeye akihaidi atawapelekea madarasa matatu kutoka ofisi ya TAMISEMI.

CHANZO: ITV
Sio Mitano tena ni milele kabisa tafadhali....
Uchumi wa kati....
Nchi hii ni tajiri sana....
Au nasema uongo ndugu zangu....
Unaijua vieite wewe..???
Sisi tunatembelea mavieitee....!!!
 
Wanasema chini ya mkorosho kuna oksijeni ya kutosha.
Mitano tenaa
 
Kuna wakati ukimsikiliza kiongozi anasema upinzani umerudisha maendeleo nyuma unasikia kichefuchefuu.
Hii ni Tanzania kweli,ndio tunapotakiwa kutembea kifua mbele?! So sad [emoji22]
 
Kuna wakati ukimsikiliza kiongozi anasema upinzani umerudisha maendeleo nyuma unasikia kichefuchefuu.
Hii ni Tanzania kweli,ndio tunapotakiwa kutembea kifua mbele?! So sad [emoji22]
Sio Mitano tena ni milele kabisa tafadhali....
Nchi hii ni tajiri sana....
Uchumi wa kati....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu....
Hapa kazi tu....

Unaijua vieite wewe??
Sisi tunatembelea mavieitee!!!
 
Back
Top Bottom