Wanafunzi Shule ya Msingi Namalombe wasomea chini ya mkorosho

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa, kutokana na shule hiyo kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

site%203.jpg

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema wanafunzi wa darasa la saba, darasa la kwanza na darasa awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili,la tatu,la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo kimoja cha nyasi walimu na wanafunzi.

site%205.jpg

Darasa linalotumika na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Hayo yamebainika baada ya ziara ya Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara Hamis Dambaya ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu,ofisi na madarasa mengine huku yeye akihaidi atawapelekea madarasa matatu kutoka ofisi ya TAMISEMI.

CHANZO: ITV
Kwa hiyo huko Nanyumbu mbunge wake anatokea upinzani?
 
Hiyo wilaya DC, DED, na Afisa elimu msingi wana kazi gani ,wanashindwa kuchangisha wananchi mchango wajenge wenyewe mambo mengine aibu kwa taifa.
 
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumehomolwa Sana Ndugu Zangu
Vyovyote Mtakavyosema Najua Mmenielewa
😀😁😂🤣🤣😃🤣🤣😄😄😅😅😅😅😄😄😃🤣😂
Leo Ile Shule Isingekwisha Ningetoa Demo
Ningefukuza Wote
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Mbunge wao alikuwa Cecil Mwambe wa Chadema?
Nadhani hata huyo Naibu Waziri alikuwa Chadema 🤔. Lakini Chadema na wapinzani kwa ujumla bado wapo? Ni wakati wa kuwasahau sasa tuendelee na ilani ya kijani ya madege, masgr, mavieite na mainterchange - wanyonge, wajinyonge!

Maendeleo yana chama kimoja tu.

cinq de plus, s'il vous plaît.
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa, kutokana na shule hiyo kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

site%203.jpg

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema wanafunzi wa darasa la saba, darasa la kwanza na darasa awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili,la tatu,la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo kimoja cha nyasi walimu na wanafunzi.

site%205.jpg

Darasa linalotumika na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.

Hayo yamebainika baada ya ziara ya Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara Hamis Dambaya ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu,ofisi na madarasa mengine huku yeye akihaidi atawapelekea madarasa matatu kutoka ofisi ya TAMISEMI.

CHANZO: ITV
Sisi tushazoea mbona hii ni hali ya kawaida
 
Back
Top Bottom