Mimi ni mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC), tumepokea Disbursement ya Boom na Tuition Fee tangu Desemba 6, 2024.
Mpaka hivi sasa (leo Desemba 30, 2024) tumepewa cheque No ya Tuition Fee imepita wiki mbili (02) lakini hadi hivi sasa hatujawekewa Cheque No ya Boom (fedha ya kujikimu).
Wanafunzi hatuna fedha za Kujikimu, zimepita siku 24 ambazo ni wiki 3 na siku 1 bila Cheque No, hali ni ngumu, tunasoma tukiwa katika mazingira magumu.
Malipo ya Tuition fee na Boom la pili yaliwekwa (disbursement) siku moja (06.12.2024) lakini Tuition fee cheque no wamesha weka na tumesha saini wiki ya pili sasa . Lakini fedha ya kujikimu (Boom) hatujawekewa Cheque no mpaka hivi sasa.
Pia soma
~ Baadhi ya wanafunzi waliopata Samia scholarship UDSM wakumbana hali ngumu kufuatia kutopata fedha za kujikimu na ada ya masomo
~ Bodi ya Mikopo yatoa ufafanuzi kuhusu Wanafunzi ambao hawajapata Fedha za Kujikimu "Boom"