#Je suluhisho la udangaji ni ndoa?.
# Una hakika wakiruhusiwa kuolewa kwa umri huo wata opt kuolewa au kudanga
Kwa kua case study ni Mtwara wacha nikujuze yafatayo kwani nimeishi Mtwara kwa miaka 9 Sasa
1. Parental care Mtwara ni Changamoto kubwa,hii inasababishwa na kutengana kwa wazazi sababu ya TALAKA,, watoto wengi wanalelewa na Bibi,mjomba au watu Baki ,,baba,& mama wakiwa busy na ndoa zao mpya zinazovunjika na kutafutwa kila.kukicha
NB it's common ka bint ka 22yrs kua kameolewa na kuachika Mara 4 au 5.
Sasa mabinti wanakosa uangalizi,,matokeo yake wanaanza vitendo vya ngono mapemaaa
Nimewahi uliza darasa lenye wanafunzi 98 Nani anakaa na baba na mama,,3 walikua wamefiwa,,10 wanaishi na wazazi wote wawili wanaobaki wote hawaishi na wazazi
2. Tamaduni,Mila na desturi za kusini
Huku Bwana kunaa kitu chaitwa jando na Unyago,,hapa vitoto vidogo vyapelekwa jandoni nakufunzwa vitu vya kikubwa ,,Tena wanaaminishwa vitu vibaya hasa watoto wa kike, baada ya hapo.inafatiwa na sherehe kubwaa watu wanakunywa wanalewa wanacheza singeli.na kuvua nguo mbele ya watu (ingia YouTube jionee) .
Sasa unapoanza kumwaminisha mtoto mdogo kua yeye utajiri wake na maisha yake yata endeshwa na sehemu zake za siri unamjengea future gani kwenye Dunia hii yenye interaction?.
NB: udangaji Mtwara si tu kwa vitoto vidogo ,,it's almost kwa kiasi kikubwa Cha wanawake wa Mtwara ,mjini na vijijini hasa kipindi Cha msimu wa korosho na Ngoma Kama Sasa hivi. Ni rahisi kupata huduma ya ngono Mtwara kuliko maji ya kunywa