Kuna baadhi ya hoja hapo nimekuelewa sana
Kama zipi
Basi kama haudanganyi Lete kifungu Cha Biblia kinachothibisha madai yako ya huo umri
Non canonical infancy Gospel of James plus a number of Ancient Jewish writtings.
Hata bible yenyewe ukiisoma vizuri katika lugha za kilatini na Amharic au hata hiyo hiyo bible yako ya kiswahili na kiingereza ina suggest she was 12 when she was pregnant for Jesus.
Why?
According to ancient Jewish tradition, msichana alichumbiwa akiwa na miaka 12 na aliolewa akiwa na miaka 13.
Mary alipata ujauzito katika kipindi cha courtship ( uchumba) kati yake na Joseph. So the scripture suggest that she was 12 when she got pregnant for Jesus.
Pia ukisoma injili ya Luka, Mariam anaanza kuwa introduced kwa kuitwa " Palikuwa na bikira mmoja alieitwa Mariam"
Bikira hapa imetumika kumaanisha msichana mdogo mwenye umri wa chini ya miaka kumi na 3 kwa sababu wasichana wa umri huo walikuwa presumed kuwa bikira.
Ndio maana sentensi inaanza na msichana bikira ambae jina lake anaitwa Mariam.
Ingekuwa tofauti kama ingeanza na msichana mmoja aitwae Mariam ambae ni bikira au msichana mmoja aitwae Mariam, huyu msichana aitwae Mariam alikuwa bikira.
Hii sentensi ya pili ina maanisha kwamba Mariam tayari ni msichana mtu mzima lakini bado ni bikira kwa maana ya kwamba ameshapita umri ule wa kuchumbiwa na hana mchumba na tayari anajulikana kwa maana ya kwamba ni mtu mzima tayari ila ni bikira.
Msichana bikira aitwae Mariam/ bikira mmoja aitwae Mariam = msichana mdogo bikira under the age of 13 . Her name is Mariam.
Palikuwa na msichana aitwae Mariam, huyo Mariam alikuwa bikira = Mariam ni mtu mzima lakini pia ni bikira.
Ni sawa na wewe mkuu binti yako wa darasa la tatu automatically tuna assume ni bikira. Hatumjui jina lake ila tuna assume ni bikira. So tukitaka kumzungumzia kwa lugha ya mwandishi wa andiko hili kwenye Biblia tutasema " kuna bikira mmoja aitwae lets say ( mwanakombo)
Ila kama una mtoto wako amemaliza chuo kikuu ila ni bikira, jamii ita assume kwamba sio bikira. So tukienda kwa lugha ya mwandishi wa Biblia tutasema " Mwanamke mmoja au msichana mmoja aitwae Mwanakombo, ambae pia ni bikira..."
Ukisoma vizuri Luka 1: 26-45 utaona bikira Maria alipo ambiwa habari za ujauzito alishtuka sana kwa sababu alikuwa mtoto na hakuwa na mume bali alikuwa na mchumba tu ambae wangeoana mwaka mmoja baadae. Na kwa umri wake alidhani aisngeweza kupata ujauzito kwamba yeye angeolewa akiwa na miaka kumi na tatu then ujauzito anaubeba akiwa na kumi na 4 na angejifungua akiwa na miaka 15.
Kwa kulijua hilo malaika Gabriel anamwambia usiwe na wasiwasi kwa sababu kuna mwanamke jamaa yako ambae ni mzee anaitwa Elizabeth yeye pia kwa uwezo wa Mungu amepata ujauzito. So hapo malaika Gabriel anamtoa hofu bikira Maria kwa kumwambia kwamba licha ya kuwa na umri mdogo lakini kwa uwezo wake Mungu atabeba ujauzito na atazaa mtoto salama.