Bishop Hiluka,
Umeweka sawa, ila sahihisha hapo pa "kikaelewa nchini Tanzania" wakati wa Mjerumani, kwanza kabisa wakati huo hakukua na kitu kinaitwa Tanzania, pili Kiswahili kiliendelea kulelewa na Wapwani wa pande zote wakiwemo Wazenji mpaka wakati Nyerere alipokikuta na kukifanya lugha rasmi ya Tanzania, ndio maana nilikua namsahihisha mleta mada aliposema Kiswahili ni cha Tanzania, ilhali tunajua Tanzania ilikikuta.
Kuhusu Kingereza kosa lenu kubwa mnaanza kukisomea sekondari, ukitaka umahiri wa lugha anza kujifunza ukiwa mdogo, akili zikiwa changa, sio unashtukizwa ukubwani halafu unategemewa uitumie. Halafu huwa naona kama ujuha fulani hivi maana Watanzania wenye hela huhakikisha watoto wao wanajifunza Kingereza wakiwa wadogo halafu wanahimiza walalahoi wa mitaani wasiokua na hela wao waendelee na Kiswahili kwenye saint Kayumba za mitaani, kisha kwenye soko la ajira inaandikwa kama mojawapo wa vigezo "must be fluent in English".
Nenda hapo Milimani City uone familia nyingi za wenye hela wakati wametoka out, ni mwendo wa kingereza kingereza, wazazi wanapambana kuhakikisha watoto wanakomaa kwenye kingereza kimya kimya, ila ukiwaskia baadaye wanakuambia wao ni wazalendo wa Kiswahili na kila mtu azungumze Kiswahili maana ni lugha ya Tanzania.
Mimi Kiswahili nakipenda sana, tena mzalendo kupita maelezo, hakuna mgeni ambaye nimefanya naye miradi yoyote na sikumfundisha Kiswahili, yaani nampa daftari kabisa aandike mambo ya msingi na namkumbushia kila wakati, ila pamoja na yote Kingereza nakitumia sana maana kinaniunganisha na dunia, hapa kwenye Skype natema yai na Wwachina na watu wa mataifa mengine bila matatizo, ila pia lugha yangu ya asili huwa siiachi, Kikikuyu kwa kwenda mbele.