Wanafunzi wa Kimarekani Wakiendesha Mdahalo wa Urais wa Tanzania kwa Kiswahili

Wanafunzi wa Kimarekani Wakiendesha Mdahalo wa Urais wa Tanzania kwa Kiswahili

Uchaguzi gani waliona watanzania wanafanya siasa za namna hiyo za kuelezea sera zao, mbinu zao or even having alternative to anything.

Ilani yenyewe ya uchaguzi watu wanapewa miezi miwili ya kuamua so far hakuna mpiga kura ata mmoja anajua ina nini, inamgusa vipi kikodi au inamsaidia vipi kimaisha na maslahi yake kutoka chama chochote.

For what is worth they are only going to be future CIA agents (disguised in IMF, WB or other policy machines that shape us) if not directly employed on their International affairs advisor acting as experts on EA politics; Mbowe anawahusu nini na somo la kiswahili.
 
Uelewa wao wa kiswahili unaridhisha! Hongereni vijana, karibuni tanzania mkinoe kiswahili chenu vizuri zaidi.
 
Wapo wanafunzi wa Edinbhurg University hapa Butiama Kwa mini mtu asiwaombe kufanya mdahalo kiswahili. Wanaondoka jumamosi.
 
A FORMAL AND A VERY PURE SWAHILI IS SPOKEN IN TANZANIA......
Nimenukuu maneno hayo katika article fulani ya jamaa mmarekani........ Alikuwa akijibu swali la mdau fulani aliyeuliza Kiswahili ni lugha ya taifa gani
 
Roberto 20 pia siku nane zilizopita nilikuwa nikiongea na wadada kutoka UK, mmoja London na mwingine Manchester. Katika maongezi huyu wa London alidai alikuwa Kenya kabla na kukiri wazi yeye kwa mtazamo wake anaona Kiswahili fasaha ni kutoka Tanzania.
 
Hehehe!! Yaani nguvu mnazotumia kwenye kulia lia kuhusu Kiswahili kuwa cha Tanzania.

Chimbuko la Kiswahili ni kabila la Wangozi kutokea Pwani ya Kenya, someni historia muache kulia lia. Muarabu alikuja akakiboresha kwa kuchomekea maneno yake mengi na pia akaongeza na maneno ya wabantu wengine hadi kikawa lugha ya Wapwani, yaani ukanda wote wa Pwani, kipindi hicho hakukua na Kenya wala Tanzania.

Watu wa mikoani kama Wasukuma, Wanyakyusa na sisi Wakikuyu tukadandia humo humo na kuendelea kukitumia na kujitambulisha nacho kama lugha rasmi, na tumeendelea kukikuza hadi kimepokewa Afrika.

Sasa badala ya kulia lia kila siku, kile mngefanya Watanzania ni kushirikiana sote tukikuze kiendelee kupokewa duniani. Sema ni vigumu kukipigia debe kama mumeganda kwenye lugha moja kwa mlivyo wazembe mumeshindwa kujifunza Kingereza, hapo inakua vigumu hata kwa walimu wenu kupata soko huko nje, hadi wamefunikwa na Wakenya.
 
MK254,
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, kwamba Kiswahili ni lugha ya Afrika Mashariki, kilianzia Pwani ya Afrika Mashariki na kikalelewa nchini Tanzania wakati wa utawala wa Mjerumani (kabla hata hatujapata uhuru) na baadaye Mwingereza akaendeleza kile alichoanza Mjerumani, kisha Nyerere akachukua mkondo huohuo. Hapa suala kubwa ni kushirikiana (kama ulivyosema) ili tukikuze na kukiendeleza badala ya kulumbana, jambo ambalo wala halikisaidii kukua.

Kuhusu suala la Watanzania na Kiingereza si kweli kwamba hatujifunzi au hatukijui, wengi wanajua Kiingereza, ongea chochote watakuelewa ila tatizo kubwa ni kwamba hawako fluent (wengi hawakiongei kwa ufasaha) nadhani kutokana na kutumia zaidi Kiswahili na lugha za makabila kwenye shughuli za kila siku, pia hawajiaminii...
 
Bishop Hiluka,

Umeweka sawa, ila sahihisha hapo pa "kikaelewa nchini Tanzania" wakati wa Mjerumani, kwanza kabisa wakati huo hakukua na kitu kinaitwa Tanzania, pili Kiswahili kiliendelea kulelewa na Wapwani wa pande zote wakiwemo Wazenji mpaka wakati Nyerere alipokikuta na kukifanya lugha rasmi ya Tanzania, ndio maana nilikua namsahihisha mleta mada aliposema Kiswahili ni cha Tanzania, ilhali tunajua Tanzania ilikikuta.

Kuhusu Kingereza kosa lenu kubwa mnaanza kukisomea sekondari, ukitaka umahiri wa lugha anza kujifunza ukiwa mdogo, akili zikiwa changa, sio unashtukizwa ukubwani halafu unategemewa uitumie. Halafu huwa naona kama ujuha fulani hivi maana Watanzania wenye hela huhakikisha watoto wao wanajifunza Kingereza wakiwa wadogo halafu wanahimiza walalahoi wa mitaani wasiokua na hela wao waendelee na Kiswahili kwenye saint Kayumba za mitaani, kisha kwenye soko la ajira inaandikwa kama mojawapo wa vigezo "must be fluent in English".
Nenda hapo Milimani City uone familia nyingi za wenye hela wakati wametoka out, ni mwendo wa kingereza kingereza, wazazi wanapambana kuhakikisha watoto wanakomaa kwenye kingereza kimya kimya, ila ukiwaskia baadaye wanakuambia wao ni wazalendo wa Kiswahili na kila mtu azungumze Kiswahili maana ni lugha ya Tanzania.

Mimi Kiswahili nakipenda sana, tena mzalendo kupita maelezo, hakuna mgeni ambaye nimefanya naye miradi yoyote na sikumfundisha Kiswahili, yaani nampa daftari kabisa aandike mambo ya msingi na namkumbushia kila wakati, ila pamoja na yote Kingereza nakitumia sana maana kinaniunganisha na dunia, hapa kwenye Skype natema yai na Wwachina na watu wa mataifa mengine bila matatizo, ila pia lugha yangu ya asili huwa siiachi, Kikikuyu kwa kwenda mbele.
 
Chimbuko la Kiswahili ni kabila la Wangozi kutokea Pwani ya Kenya, someni historia muache kulia lia. Muarabu alikuja akakiboresha kwa kuchomekea maneno yake mengi na pia akaongeza na maneno ya wabantu wengine hadi kikawa lugha ya Wapwani, yaani ukanda wote wa Pwani, kipindi hicho hakukua na Kenya wala Tanzania.
Dola ya kilwa iliyodondoka karne ya 12 walikuwa wakiongea kiswahili, sasa hiyo Kenya imetoka wapi?
 
Dola ya kilwa iliyodondoka karne ya 12 walikuwa wakiongea kiswahili, sasa hiyo Kenya imetoka wapi?

Soma historia wacha uzembe bro, vitabu vipo.
Mimi nazungumza kuhusu kabila la Wangozi lililokuwepo tangu, hata kabla mwarabu hajaja kubuni hiyo dola.
 
Roberto 20 pia siku nane zilizopita nilikuwa nikiongea na wadada kutoka UK, mmoja London na mwingine Manchester. Katika maongezi huyu wa London alidai alikuwa Kenya kabla na kukiri wazi yeye kwa mtazamo wake anaona Kiswahili fasaha ni kutoka Tanzania.
Kweli kiongozi....... Ndo inavyojulikana hivyo
 
Back
Top Bottom