KERO Wanafunzi wa MASTERS na Ph.D Hosteli za Ubungo - UDSM tunanunua maji ndoo moja Tsh. 1,000

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kumekuwepo na ukosefu wa maji katika Hostel za Ubungo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapoishi Wanafunzi wa Uzamili (Postgraduate Students) ambao tunasoma Master's Degrees na Ph.D!

Kipindi hiki hali imekuwa mbaya zaidi na tunalazimika kununua dumu moja la Lita 20 kwa Tsh. 1,000 ambayo ni sawa na ndoo moja, Wakazi wa Hostel tukiuliza uongozi wa Wanafunzi na Warden wa Hostel wanatuambia lipo nje ya uwezo wao.

Hali hiyo inatusikitisha sana hasa kwa kuwa sisi ni wapangaji tunaostahili kupatiwa huduma zote muhimu ikiwemo maji.
Kero hii ni ya muda mrefu, soma pia hapa: KERO - Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa
Nina mpango wa kusoma PhD hapo. Hebu nijulishe tatizo litakapoisha
 
Ndoo moja buku? Wakati unit moja ya Maji 1,600.

Na unit moja ni zaidi ya ndoo 50.
 
Kumekuwepo na ukosefu wa maji katika Hostel za Ubungo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunapoishi Wanafunzi wa Uzamili (Postgraduate Students) ambao tunasoma Master's Degrees na Ph.D!

Kipindi hiki hali imekuwa mbaya zaidi na tunalazimika kununua dumu moja la Lita 20 kwa Tsh. 1,000 ambayo ni sawa na ndoo moja, Wakazi wa Hostel tukiuliza uongozi wa Wanafunzi na Warden wa Hostel wanatuambia lipo nje ya uwezo wao.

Hali hiyo inatusikitisha sana hasa kwa kuwa sisi ni wapangaji tunaostahili kupatiwa huduma zote muhimu ikiwemo maji.
Kero hii ni ya muda mrefu, soma pia hapa: KERO - Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa
Mwanafunzi wa masters na PhD kuishi hostel ni aibu.

Ina maana mpaka pesa ya kwenda kupanga inawashinda mpaka mng'ang'anie muishi boarding?
 
Unasoma PhD unakaa hostel?

Acha utoto, kama si mkazi wa Dar tafuta nyumba upange. Panga nyumba yenye mahitaji yote muhimu, kama unaishi kwa kujibana tafuta wenzako 'those you cordially click with' mchange pamoja mpange nyumba.
Hata kuchanga ili muishi pamoja ni utoto .

Hayo wawaachie first year wa undergraduate.
 
Back
Top Bottom