A
Anonymous
Guest
Wanafunzi wa MUST Mbeya Tunaomba Majibu Kuhusu Kuchelewa kwa Boom ya HESLB kwa Watumiaji wa CRDB
Tunapaza sauti yetu kama wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kuhusu changamoto kubwa inayotukabili kwa sasa.
Ni takribani wiki ya pili sasa baadhi ya wanafunzi wanaotumia akaunti za CRDB bado hawajapokea fedha za kujikimu (Boom) kutoka HESLB, wakati wanafunzi wanaotumia baadhi ya benki nyingine tayari wameanza kupokea.
Tunajiuliza, changamoto iliyopo ni nini hasa? Kwa nini kundi hili la wanafunzi limeachwa nyuma bila maelezo ya wazi?
Hali imekuwa ngumu sana kwa wanafunzi wengi ambao wanategemea fedha hizi kwa mahitaji ya msingi kama chakula, usafiri, malazi pamoja na michango ya ada. Wengine wamefikia hatua ya kushindwa hata kupata mlo wa siku.
Kinachoongeza huzuni ni kwamba tunapojaribu kufuatilia kupitia mamlaka husika, hatupati majibu yanayoeleweka wala taarifa rasmi kuhusu lini tatizo hili litapatiwa suluhisho.
Wiki ijayo tunaanza Test 2, hivyo hofu kubwa imeongezeka kwa wanafunzi ambao bado hawajamaliza taratibu za ada kutokana na kuchelewa kwa fedha hizi.
Tunaomba HESLB, uongozi wa MUST na mamlaka husika kutoa ufafanuzi wa haraka:
Wanafunzi tunahitaji majibu, uwazi na hatua za haraka.

- Tatizo la kuchelewa kwa malipo kwa watumiaji wa CRDB ni nini?
- Ni lini wanafunzi hawa watapokea fedha zao?
- Kwanini hakuna taarifa rasmi inayotolewa kwa wanafunzi?