Ujenzi Tanzania
Member
- Mar 28, 2026
- 25
- 37
Sisi ni wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), ambao baadhi yetu tumehitimu mwaka 2026 na wengine tunaingia mwaka wa tatu. Tunatoa malalamiko kuhusu fedha tulizolipa kwa ajili ya mafunzo ya udereva na upatikanaji wa leseni, ambazo hadi sasa hatujapata huduma tulizolipia.
Wakati tukijiandaa na mitihani ya mwisho, mhadhiri wa NIT alifika chuoni na kutangaza ofa ya mafunzo ya udereva ambayo yangeambatana na upatikanaji wa leseni. Kwa kuwa alitumia utambulisho wa chuo, wanafunzi wengi tulimwamini na kumkabidhi fedha kwa ajili ya mafunzo hayo na leseni.
Hata hivyo, sasa imepita takribani miezi minne bila kupata huduma tulizoahidiwa. Aidha, wanafunzi wengi walipata mafunzo kwa muda mfupi sana, baadhi yetu kwa siku tatu hadi tano pekee, jambo linalozua wasiwasi kuhusu ubora na ukamilifu wa mafunzo hayo.
Baada ya kuanza kufuatilia fedha na huduma tulizoahidiwa, mawasiliano kupitia makundi ya WhatsApp yalikatishwa, na maelezo kuhusu taratibu za polisi na mifumo ya kupata leseni na vyeti yakaanza kutolewa. Hali hii imeongeza wasiwasi miongoni mwa wanafunzi waliohusika.
Kwa mujibu wa wanafunzi, walioathirika ni zaidi ya 100. Tunaziomba mamlaka husika, ikiwemo uongozi wa NIT, TRA na Jeshi la Polisi, kufuatilia suala hili, kuchunguza madai yaliyotolewa na kuhakikisha kuwa haki za wanafunzi zinalindwa.
Tunasisitiza kuwa tunahitaji ufafanuzi wa wazi kuhusu fedha tulizolipa, utekelezaji wa mafunzo tuliyoahidiwa na upatikanaji wa leseni. Ikiwa huduma hizo haziwezi kutolewa kama ilivyoahidiwa, tunaomba fedha zetu zirudishwe kwa utaratibu unaostahili.
Tunaomba suala hili lichukuliwe kwa uzito ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.