Ni Asubui ya saa 12 naelekea zangu kituo cha daladala ili niwai kazini,pembezoni mwa barabara naona watoto wawili wa kike wamesinzia na kulaliana.Mdogo kamlalia mkubwa mapajani,mkubwa kajiegemeza kwenye ukuta.Niliwafikia nikamuona mdogo kavaa sare za shule ila mkubwa kavaa nguo za nyumbani na pembeni kuna begi la shule.Ikabidi niwaguse nijue kulikoni,uku wakipiga miayo mkubwa akanambia wanasubiria gari ya shule (school bus).kuwahoji vizuri yule mkubwa ni dada wa kazi kamsindikiza mtoto kupanda gari la shule.
Tukio ili lilinifikirisha sana na kuniacha na maswali mengi kuhusu malezi na ustawi wa watoto wetu na maendeleo yao kielimu. Ni ukweli usiofichika kwamba,
Watoto wengi wanaamka alfajiri au asubui sana ili wawai kwenda mashuleni. Watoto wanaopelekwa na magari shuleni ndio wanakua wahanga wakubwa sababu inabidi wadamke asubui sana ili kuwai gari la shule lisiwaache.Kama watoto hawa nilikutana nao saa 12 asubui ina maana wameamka saa 10 au 11 alfajiri ili wajiandae kwenda shuleni. Hii ina maana watoto hawa wanakosa muda wa kutosha wa kulala na kupumzisha mwili.
Ni mara nyingi tu asubui unapanda daladala unakuta watoto wa shule wamesinzia kwenye viti au unaona school bus limejaa watoto wamesinzia,hii ina maana watoto wanaamka mapema sana ili kuwai masomo yanayoanza saa mbili kamili asubui.
Kuna wale wanafunzi ambao wanaishi mbali na shule,hawa ndio uwa wa kwanza kuchukulia na school bus na ndio wa mwisho kurudishwa nyumbani, hawa ndio unakuta saa 12 kasoro asubui wapo barabarani wanasubiria usafiri wa shule.
Utaratibu huu wa kuwaamsha watoto asubui sana napna una athari katika ukuaji wao,afya zao na hata katika maendeleo yao kielimu kwani mtoto asiepata muda wa kutosha wa kupumzika hawezi kua na maendeleo stahiki.Pia kudamka mapema kiasi icho ni hatari kwa usalama wao.
Ushauri wangu kwa serikali ni kubadilisha muda wa masomo kwa wanafunzi wa chekechea na shule za msingi,muda wa masomo uanze saa tatu kamili asubui mpaka saa tisa alasiri tofauti na sasa wanasoma kuanzia saa mbili asubui mpaka saa nane mchana. Kwa kusogeza mbele muda wa kuanza masomo ninaimani kutawapa nafasi watoto wetu kupumzika vya kutosha na kutoamka mapema alfajiri ili kuwai masomo.nina imani masomo yakianza saa tatu asubui basi wanafunzi wataanza kwenda mashule kuanzia saa moja asubui muda ambao ni mzuri kwa umri wao.
Nina imani wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo wizara ya elimu,or-tamisemi,taasisi ya elimu,kamishina wa elimu na umoja wa wamiliki wa shule binafsi wanaweza kukaa chini na kulichakata jambo ili kwa masilai mapana ya watoto wetu.kusogeza mbele muda wa masomo kutaongeza tija kwa watoto wetu katika kujifunza na pia katika ukuaji wao na pia kuongeza ufanisi kwa wanaohusika na kuwafikisha watoto hawa mashuleni