Wanafunzi wa shule za upili Tanzania wajionea mvuto wa utamaduni wa China

Wanafunzi wa shule za upili Tanzania wajionea mvuto wa utamaduni wa China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Juni 20, wanafunzi wa shule za upili wa Tanzania walioshiriki kwenye kambi ya majira ya joto ya Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) walijionea kwa undani mvuto wa urithi wa utamaduni usioshikika wa China. Shughuli hiyo ya kiutamaduni iliyoandaliwa na Chuo cha Utamaduni wa Kimataifa na Maendeleo ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, ilihusisha uchoraji wa michoro ya Mwaka Mpya wa jadi wa China kwenye ubao, uandishi wa maandiko ya kale ya kwenye mifupa na utengenezaji wa vinyago vya udongo vya jadi vya “Ninigou”.

Michoro ya mwaka mpya wa jadi kwenye ubao ikiwa ni moja ya sanaa za urithi wa utamaduni usioshikika wa China, inabeba matarajio mema ya wachina kwa siku zijazo. Mwalimu kutoka Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Chen Yingjie aliwafahamisha wanafunzi hao kuhusu historia ya sanaa hiyo na jinsi michoro hiyo ilivyotengenezwa. Baadaye wanafunzi pia walijaribu wenyewe kutengeneza michoro yao ya mwaka mpya wa jadi wa China.

1687935736980.png

(Wanafunzi kutoka Tanzania wanasikiliza kwa makini maelezo ya mwalimu Chen Yingjie kuhusu namna ya kutengeneza michoro ya mwaka mpya kwenye ubao)

1687935758389.png

(Mwanafunzi anaonesha kazi zao za michoro ya mwaka mpya.)

Maandiko ya kale kwenye mifupa mifupa ni maandiko ya kale zaidi yaliyogunduliwa duniani. Maandiko hayo yanayoonekana kama mchanganyiko wa maneno na michoro yamewavutia sana wanafunzi hawa kutoka Tanzania. Baada ya kufahamishwa namna ya kuandika maandiko hayo, walijaribu kuandika majina yao ya Kichina kwa mtindo wa maandiko hayo ya kale.


1687935816357.png

(Mwalimu Zhang Zeping anawaelekeza wanafunzi kuandika majina yao ya kichina. )



Vinyago vya udongo vya “Ninigou” ni vitu vya jadi vya kuchezea vilivyotengenezwa kwa udongo kutoka mji wa Zhoukou mkoani Henan. Vinyago hivyo vinavyobeba ibada za kale vimetajwa na wataalamu kama“visukuku hai vya jamii za kale za China, na vimejumuishwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China. Mwalimu Chen aliwafundisha wanafunzi namna ya kupaka rangi kwenye vinyago hivyo, na baada ya kumaliza, walionesha kazi zao kwa furaha.

1687935838342.png



(Mwanafunzi wanaonesha kazi zao za vinyago vya udongo vya Ninigou. )
 
Back
Top Bottom