Tukio tukio limefanyika katika Shule ya Sekondari Karibuni ambapo DC Jokate ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa madarasa na ametoa wito kwa Wazazi kuendelea kuwahimiza Watoto wao kwenda Shule.
"Nafarijika kuona muitikio wa Wazazi kuwapeleka Watoto wao kujiandikisha umekuwa mkubwa na hii imetokana na hamasa iliyoanzishwa na Rais Samia, ameonesha kipaumbele ameonesha moyo wake upo kwa Watoto, kwa Vijana na kwenye Jamii, leo tumekuja kuwaonesha kuwa maono ya Rais Samia yametimia"
"Ujenzi wa vyumba vya madarasa 157 haijawahi kutokea kwa wakati mmoja ni mradi tulioukamilisha ndani ya muda mfupi wa miezi miwili, kama Wilaya tutaendelea kumuunga mkono Rais kwa vitendo"
My take: Mkopo huu umetumika vizuri, hata sisi wenyewe tunapokopa kwenye vikoba ili tujenge siku ukimaliza nyumba unakuwa unalipa mkopoa ambao matokeo yake unayaona.
Bongo unakuta mtu anasema eti mkopo haufai.