Ni kweli Mkuu kinachotakiwa ni elimu mahsusi zitolewe kuhusu Internet kiujumla hii inabidi ianzie ngazi za chini kuwashape vijana,japo itakua ngumu ila itasaidia mbeleni zamani Wakati ugonjwa wa UKIMWI unaingia bongo watu walificha maradhi na kuwalisha sumu mbaya vijana na watoto eti
Ni ugonjwa wa kurogwa wengi wakafia Kwa waganga wa kienyeji wakiaguliwa wakidhani wamelogwa kumbe sivyo,
Ilipokuja swala la elimu ya kujikinga watu walipoambiwa watumie kondom ilikua kama dhambi kutamka neno kondom Kwenye Jamii madhara yake tukapoteza ndugu zetu wengi Kwa kukumbatia fikra mfu na za kijinga Tena wengine wakiwa wasomi kabisa walishindwa toa taarifa sahihi Kwa Jamii
Mpaka Leo madhara tunayaona ya ule uzembe,
Pia kuhusu Hilo la simu mashuleni iwe ni Moja ya Elimu na Kwa vitendo maana vijana wengi wakitoka Huko mashuleni
Na kwenda chuo kitu Cha kwanza hua ni kumiliki simu janja kutokana na ukosefu wa exposure na Elimu kuhusu Internet kiujumla
Madhara yake zinageuka Camera za kurekodia video za ngono,kubase Kwenye kufuatilia mambo ya kipumbafu,kuwaingiza Kwenye maisha fake wanayoyaona mtandaoni hasa Kwa mabinti na vijana mwishowe huingia Kwenye vishawishi vya ngono na kujiuza
Nadhani unalijua balaa la watoto wa chuo na uchafu wao Kwenye mitandao mfano
Wazeee wa konection SI unawajua😁😁🔥🔥
Ile yote ni madhara ya kuzuia vitu ambavyo inawapasa wavijue Kwa Muda mwafaka wakiwa Bado wabichi endapo wangekua wameiva Toka udogoni Kwa kuchukulia ni swala la kawaida hata isingekuja kua nongwa wakifika stage ya kutumia maana Wana Elimu sahihi itakayowasaidia kuchuja mambo!