Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu, wafyeka shamba kisa adhabu ya kukutwa na simu shuleni

Shule za serikali ni utopolo tu hiyo nguvu walimu wa nidhamu wanayoitia kwa Wanafunzi wangedirect katika academics ingewatosha kufaulisha.

Unakuta Mwalimu haingii mwezi mzima darasani, unaingia mitihani ya Taifa kuna topics hujawahi kufundishwa (unaomba Mungu usikutane na swali la topics ambazo hujasoma), kuna practicals hujawahi fanya na Mwalimu husika haulizwi wala kuwajibishwa wao wapo kukimbiza wanafunzi kuishi kama digidigi tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] povuuu jingi mno mwalimu kwani shida nn? Mwanafunzi kuwa na cm inahusiana vipi na kufeli masomo? Au matokeo mabaya?

Unailinganisha St Francis na Iyunga Tech uko sawa wee? Unaona zinaendana kwa kila kitu? Poleeeeeeeeeh
 
Kwa ulivyoandika unaonyesha unapendelea wanafunzi wamiliki siku mashuleni,wazitumie kadri ya akili zao zitakavyowatuma.Una maono mazuri sana,hongera.
Kumiliki cm ni kawaida kwa mwanafunzi wa A level, mie nilikua namiliki ila nliwekaga kwa mwalimu, siku za weekend ananipa natumia kwa kadri ya nitakavyo.
Ahsanteeeeeh sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] walimu wa shule za serikali hasa wa Advance, muda wa kufundisha hawana, wako kutwa kuwaambia wanafunzi nyie n wakubwa mnajitambua mjitafutie material wako kutwa kuwazabua wanafunzi tena wanavyokua na stress za mshahara kiduchu ndo kabisaa tafrani tupu, woiiiiiiiiih
 
Usikilize maelezo ya mwanfunzi akueleze A to Z vizuri labda hujawah kudill nao hao viumbe tena mtoto wa form six mvulana
 
Shule za serikali ni utopolo tu hiyo nguvu walimu wa nidhamu wanayoitia kwa Wanafunzi wangedirect katika academics ingewatosha kufaulisha.
Mwalimu kuweka Juhudi anahitaji ushirikiano wa wanafunzi sasa anaadhibu tu mtoto kwa kuvunja sheria kwa kukutana na simu mwalimu.anachomewa na kuharibiwa Mali zake unategemea awekeze nguvu kufundisha? Na walimu wengine wakiona hivyo unategemea wawe na morale wa kufudisha?

Mwanafunzi nidhamu ikiwa juu uwezekano wa mwalimu kuwa motivated kufundidha mkubwa

Mfano pita shule ya Serikali ya sekondari uone ulivyo na mikelele ya wanafunzi wengine mwalimu anafundisha darasa lingine mikelele.Lakini nenda shule za private zinazofaulisha sana muda wowote ukipita karibu waweza dhani hakuna wanafunzi kuko kimya kila mmoja ana agenda moja kusoma.kelele marufuku kwenye compound ya shule na madarasani kusikia sauti ni mwalimu akifundisha tu
 
Hujui shida yake do one thing at a time if you want to succeed in life simu ina divert hilo

Umeenda kusoma kasome simu achana nayo hata makazini ofisi nyingi serious simu yako utaiona ukitoka kazini.Muda wa kazi ni kazi tu
Shule zinazofaulisha sana wana marufuku mbili moja marufuku mtoto kwenda kusoma tuition wakati wa likizo na kusoma online kwenye simu au komputa wanasema atajichanganya walimu wanajiamini kuwa kile walichowafundisha watoto kinatosha wasije changanywa bure huko tuition au online za simu au komputa

Kwa wasoma shule za kayumba kuelewa marufuku hii ya simu inakuwa ngumu sababu huko wanafunzi wanajilea wenyewe na ujuaji wao waliotoka nao kwao kwenye umaskini mkubwa
 
Msimtetee hamumjui na sio kurekebisha yeye alikua anakuharibia hakuna msamaha wala kukosea kwa bahati mbaya ukiingia kwenye 18 zake imekula kwako.
Hata wewe ukiwa Mwalimu kuna Wanafunzi watakuita mnoko,hata km una nia nzuri na wao.
 
Kweli kabisa Mkuu, Wanafunzi wa Shule za Serikali wana shida sana kwenye suala la nidhamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…