Wanafunzi wakaidi na waanzilishi wa fujo wa Shule ya Sekondari Mpwapwa, Dodoma wachoma matranka na nguo za wanafunzi wenzao

Wanafunzi wakaidi na waanzilishi wa fujo wa Shule ya Sekondari Mpwapwa, Dodoma wachoma matranka na nguo za wanafunzi wenzao

chakutu

Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
69
Reaction score
62
Wakaidi hao Wanajigamba hakuna Mwalimu yeyote wala Mkuu wa Shule anayeweza kuwafanya chochote, Mpaka sasa Wanafunzi wanaendelea na Masomo.

Ninachojiuliza ni hivi kama wangeunguza Mabweni ingekuwaje ? Mali zote za shule kongwe kwa kweli zingeungua pamoja na Vifaa vyao
 
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mpwapwa – Dodoma wamechoma matranka na nguo za wanafunzi wenzao.
baada ya viongozi wa wanafunzi kutoelewa na wanafunzi wenzao
 
Duuuu, mimi mwenyewe nimeisikia hii issue, alafu Mkuu wa Shule nasikia anawaogopa hao wanafunzi, nasikia anawahamasisha wanafunzi wasiende kusema kwa wazazi juu ya tukio lililotokea, huu ni uboya.

Enzi zetu hapo mwanafunzi ushashapwa viboko vyako matakoni na saspesheni juu, lakini wanafunzi wa siku hizi wana raha kweli unaendelea na Masomo tu, hiki kizazi !!!!
 
Vyeti vya mkuu wa shule viangaliwe
Usikimbilie kusema hivyo. Pengine yeye kama Katibu wa Bodi ya Shule alishaishauri Bodi iwafukuze hao wapuuzi ila Bodi ikaendelea kuwalinda kwa mujibu wa sheria na taratibu za kipuuzi zilizopo.

Siku hizi mitoto inawatetezi wengi mno kiasi kwamba ukiamua kuchukua hatua wewe Mkuu wa Shule ndo unaonekana mbaya mbele ya wadau wote wa elimu. Just imagine lile toto la Mbeya lililosababisha Mwl.Jimmy atukanwe na kila mtu mitandaoni.
 
Labda ni vidato vya mtihani hao huwa wagumu sana kuchukuliwa sheria ila ni muhimu kuchukua hatua maana wanaweza hatarisha usalama wa wenzao na shule
 
Labda ni vidato vya mtihani hao huwa wagumu sana kuchukuliwa sheria ila ni muhimu kuchukua hatua maana wanaweza hatarisha usalama wa wenzao na shule
Inasemakana ni kidato cha Tano na baadhi ni kidato cha sita.
Halafu Wziri mwenye dhamani ametulia tu, wanataka mpaka shule zetu ziungue.
 
Yaani labda kuna ushahidi dhahiri kabisa,wa hao madogo kuchoma vitu vya wenzao,halafu WAOGOPWE kuchukuliwa hatua?
Uongozi wa hiyo shule,unaonyesha udhaifu sana.
 
Back
Top Bottom