Tetesi: Wanafunzi waliotimuliwa UDOM kuungana na BAVICHA tarehe 23 Julai

Tetesi: Wanafunzi waliotimuliwa UDOM kuungana na BAVICHA tarehe 23 Julai

Miaka inavozidi kwenda ndo watu wengi zaidi wanazidi kuchukizwa na ccm.Itaanguka tu,mtaona mbeleni huko.
 
Hawana hoja yyt ya msingi!Kama wao sio vi la za na wana sifa waende Mahakamani na watarudishwa!!Kichefu chefu zaidi wanapo niambia kuwa dada zetu walijiuza kupata hela ya chakula-Nosense at all
 
Hao waliojiuza ili kupata hela ya kula na nauli kwani zile fedha za boom walizopewa walifanyia nini mpaka wakawa hawana hela kabisa kufikia hatua ya kujiuza?au walikuwa ndo mambo yao ya kujiuza siku zote?

Hata hivyo naiomba serikali iwatupie Jicho la huruma hawa watoto ili wale wenye sifa watafutiwe namna ya kuendelea na masomo yao!!
Siungi mkono mfumo uliotumika kuwaondoa chuoni

Lakini vilevile siungi mkono swala la kujiuza kama kisingizio cha kukosa pesa ya nauli
-akili ku mkichwa
 
Hawana hoja yyt ya msingi!Kama wao sio ****** na wana sifa waende Mahakamani na watarudishwa!!Kichefu chefu zaidi wanapo niambia kuwa dada zetu walijiuza kupata hela ya chakula-Nosense at all
Ccm kutatua matatizo ya wananchi ni hisani lazima kwa kuwa walitwaa madaraka kwa mizengwe
 
NA SISI SPECIAL DIPLOMA TUNAELEKEA DODOMA 23.

Tunapenda kuwashukuru wazazi na wabunge wote ambao waliotusapoti katika kipindi kigumu cha kuondolewa katika masomo yetu.

Vile vile tunapenda kuchukua mda huu kulaani kitendo cha Serikali kutuondoa chuoni kama mbwa kwa kupewa masaa 24 bila nauli au hela ya kula.

Kiukweli tulifanyiwa ukatili wa hali ya juu ambao ulikuwa ni kinyume cha utawala bora na haki za binadamu.

Dada zetu wamejiuza siku hiyo ili wapate chakula wameondoka na magojwa yasiyotibika kwa sababu ya uzalendo wetu wa kuacha kuendelea na kidato cha 5 na 6 ili tulisaidie taifa letu upungufu wa waalimu wa masomo ya sayansi.

Wazazi wetu wabakia mafukala kwa sababue ya kuuza mashamba yao, ng`ombe zao pamoja kuuza vyakula ghalani kwa sababu ya matarajio yao kuwa sisi tuenda kwenye mfumo ya ajira tutawatunza ila sasa wapata tamaa kabisa.

Sisi tumepoteza mda bure sasa hivi tupo tu mtaan hatujui tunaenda wapi tumeitwa ****** lakini sisi sio ****** kabisa hata tukileta vyeti vyetu sisi vipanga kuliko hata ***** ambae tumemuacha Udom anasoma sema tu sisi wazazi wetu ni wanyonge maskini.

23 July na sisi tutakuwa dodoma kuungana na watanzania wote pamoja na wazazi wetu kifanya mambo yafuatayo;

*Moja*kutoa kilio chetu na maumivu yetu kwa Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa ccm taifa juu tulivyonyanyasika na kudhalilisha katika zoezi la Operation tumua watoto wa maskini kwa jina lingine tumeitwa ******.

Tunakuja kumuambia umaskini wa wazazi wetu ndio umetufanya tuitwe ****** na kipindi cha kuomba kura rais aliomba kura mpaka kwa ****** hakuomba kwa vipanga tu.

*Pili*Kupeleka kilio chetu kwa mawaziri wa ccm wa awamu ya nne na kuwauliza ni kwa nini hawakumshauri rais kikwete kuachana na programme hii maana jukumu la rais ni kumshauri rais kwa maana hiyo hata rais wa awamu ya sasa nae alishindwa alikuwa waziri wa ujenzi.

*Tatu*kupeleka kilio chetu kwa wabunge wa ccm ambao walikuwa wengi bungeni kuruhusu programu hii ya special diploma kuengelea na sasa kutugeuka na kutuacha tukifukuzwa kama mbwa na kulala stendi mpaka wabunge wa ukawa kuja kututetea na kututafutia sehemu pa kulala na chakula.

Kuomba hela yetu makazi tuliolipia 182500 na hela ya TCU 20000 na 5000 ya serikali ya wanafunzi walioshindwa kututetea tumesikia tu udomasana daruso ya udsm lakini nyinyi mkaa kimya yetuyetua tuwatuwapeiwalitutetea nyinsa
*Mwisho* kukabidhi kadi zetu za ccm na za ndugu zetu kama vile mama, baba mjomba shangazi kaka dada na nyinyink kwa mwenyekiti mpya atakae chaguliwa ili kuonyesha maumivu yetu na ndugu zetu kwa unyanyasaji huo tuliofanyiwa.

Vile kuiomba serikali kuturudisha udom ili tumalizie masomo yetu ili tusiwe tumepoteza mda bure maana tumefukuzwa sisi ni kwa sababu ya walimu wetu kudai mshahara yao sio kweli sisi tulikuwa ******.

Special diploma wote 7000 tunaomba tukutane dodoma tarehe 22 ili tujue hatma yetu tarehe 23 July Kwenye mkutano mkuu wa ccm asubuhi na mapema.

UMOJA NI NGUVU

By uongozi
Pia usisahau na ombaomba, madada poa, wabwia shisha na mashoga WA DAR ES SALAAM....vile vile wauza unga, na watumishi wote ambao wako benchi kwa kutumbuliwa....
 
Ningewashauri badala ya kuharibu muda wenu kwenda Dodoma mkutane kivyenu mkusanye pesa mtafute lawyer mzuri mwende mahakani acheni mambo ya siasa nafikiri that's the only solution kupata haki zenu.
 
Sidhani kama itawasaidia kupata haki yenu. Jaribu kutumia mahakama! I am convinced that this is the best option to justice

Umesema la maana....watumie mahakama kudai kile wanachoona ni haki yao...wakitumia ubabe wataumia...hata hao Bavicha nao wataumia...wasidanganywe na wanasiasa waliopanga kuwatumia vijana hao katika harakati zao...
 
Hao waliojiuza ili kupata hela ya kula na nauli kwani zile fedha za boom walizopewa walifanyia nini mpaka wakawa hawana hela kabisa kufikia hatua ya kujiuza?au walikuwa ndo mambo yao ya kujiuza siku zote?

Hata hivyo naiomba serikali iwatupie Jicho la huruma hawa watoto ili wale wenye sifa watafutiwe namna ya kuendelea na masomo yao!!
Kumbuka walifukuzwa huku zimebaki siku tatu waingiziwe boom ,hilo boom wangelitoa wap ??
 
Mnapata wapi hela za kwenda Dodoma?
Wana hela za kwenda Dom lkn hawatumii hizo hela kuboresha huduma mbalimbali kwenye majimbo yenu mnazitumia kwenda kutafuta kipigo Dom ili tu muonekane kwenye vyombo vya habari huo ni ubishololo na unafiki.
 
Kwanza poleni na maswahibu yaliyowakumba, kwa niliivyoona nchi ilikuwa inaelekea pabaya, hii sekta ya elimu imeyumbishwa sana lakini vyote ilikuwa kutafuta umaarufu, na kama tungeendelea hivi ingefika kipindi mtu anamaliza darasa la saba anazama chuo kikuu, Embu niambie tungecompete vipi soko la ajira in relation to other countries? Mie Naona badala ya kupoteza mda kwenda Dodoma kaenda na mwandikieni raisi barua ya wazi kuomba awape mwelekeo coz tayari you are lost alot of time, si ajabu mkapelekwa vyuo vya diploma mkaendeleze vipaji vyenu. Nawashauri tena msithubutu kwenda kuchokoza nyuki MTATOKA manundu maana hakuna namna nyingine
 
mliambiwa shule bure lakini inabidi tuchangie madawati, baadae tutaambiwa tuchangie vitabu,baadae tutaambiwa tuchagie chakula,baadae tutaambiwa tuchangie fedha za masomo ya zaida. walewale waliosema Elimu bure ndio wanaotutaka tuchangie. hivyo walewale waliopanga mpango wa kusoma maalum kwa sababu ya kuondoa huaba wa walimu ndio waliokufukuzeni
 
Hiyo itakuwa athari ya kuacha vijana wasio na ajira au shughuli maalumu mitaani.Ni hatari,si mijini hata vijijini makundi haya yanaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa kukata misitu kuchoma mkaa ili kupata fedha.Madhara ya kuwapa wanafunzi elimu nusunusu bila kufikia malengo yao ni hatari.Vijana kwa kukosa shughuli rasmi za kufanya wanaweza kutumiwa hata na makundi mengine ya kiharamia kwa gharama yoyote ili yatimize malengo yao.Hii ni hatari kuacha vijana bila ajira mitaani.
 
Hiyo itakuwa athari ya kuacha vijana wasio na ajira au shughuli maalumu mitaani.Ni hatari,si mijini hata vijijini makundi haya yanaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa kukata misitu kuchoma mkaa ili kupata fedha.Madhara ya kuwapa wanafunzi elimu nusunusu bila kufikia malengo yao ni hatari.Vijana kwa kukosa shughuli rasmi za kufanya wanaweza kutumiwa hata na makundi mengine ya kiharamia kwa gharama yoyote ili yatimize malengo yao.Hii ni hatari kuacha vijana bila ajira mitaani.
 
Mnapata wapi hela za kwenda Dodoma?
Hata mimi nimejiuliza hilo swali. Mleta mada kasema dada zao walijiuza ili wapate hela za kula na nauli na wameondoka na magonjwa yasiyotibika, sasa waliendelea kujiuza ili wapate hiyo hela ya kukusanyika tena dodoma tar 22?
 
Back
Top Bottom