Tetesi: Wanafunzi waliotimuliwa UDOM kuungana na BAVICHA tarehe 23 Julai

Tetesi: Wanafunzi waliotimuliwa UDOM kuungana na BAVICHA tarehe 23 Julai

NA SISI SPECIAL DIPLOMA TUNAELEKEA DODOMA 23.

Tunapenda kuwashukuru wazazi na wabunge wote ambao waliotusapoti katika kipindi kigumu cha kuondolewa katika masomo yetu.

Vile vile tunapenda kuchukua mda huu kulaani kitendo cha Serikali kutuondoa chuoni kama mbwa kwa kupewa masaa 24 bila nauli au hela ya kula.

Kiukweli tulifanyiwa ukatili wa hali ya juu ambao ulikuwa ni kinyume cha utawala bora na haki za binadamu.

Dada zetu wamejiuza siku hiyo ili wapate chakula wameondoka na magojwa yasiyotibika kwa sababu ya uzalendo wetu wa kuacha kuendelea na kidato cha 5 na 6 ili tulisaidie taifa letu upungufu wa waalimu wa masomo ya sayansi.

Wazazi wetu wabakia mafukala kwa sababue ya kuuza mashamba yao, ng`ombe zao pamoja kuuza vyakula ghalani kwa sababu ya matarajio yao kuwa sisi tuenda kwenye mfumo ya ajira tutawatunza ila sasa wapata tamaa kabisa.

Sisi tumepoteza mda bure sasa hivi tupo tu mtaan hatujui tunaenda wapi tumeitwa ****** lakini sisi sio ****** kabisa hata tukileta vyeti vyetu sisi vipanga kuliko hata ***** ambae tumemuacha Udom anasoma sema tu sisi wazazi wetu ni wanyonge maskini.

23 July na sisi tutakuwa dodoma kuungana na watanzania wote pamoja na wazazi wetu kifanya mambo yafuatayo;

*Moja*kutoa kilio chetu na maumivu yetu kwa Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa ccm taifa juu tulivyonyanyasika na kudhalilisha katika zoezi la Operation tumua watoto wa maskini kwa jina lingine tumeitwa ******.

Tunakuja kumuambia umaskini wa wazazi wetu ndio umetufanya tuitwe ****** na kipindi cha kuomba kura rais aliomba kura mpaka kwa ****** hakuomba kwa vipanga tu.

*Pili*Kupeleka kilio chetu kwa mawaziri wa ccm wa awamu ya nne na kuwauliza ni kwa nini hawakumshauri rais kikwete kuachana na programme hii maana jukumu la rais ni kumshauri rais kwa maana hiyo hata rais wa awamu ya sasa nae alishindwa alikuwa waziri wa ujenzi.

*Tatu*kupeleka kilio chetu kwa wabunge wa ccm ambao walikuwa wengi bungeni kuruhusu programu hii ya special diploma kuengelea na sasa kutugeuka na kutuacha tukifukuzwa kama mbwa na kulala stendi mpaka wabunge wa ukawa kuja kututetea na kututafutia sehemu pa kulala na chakula.

Kuomba hela yetu makazi tuliolipia 182500 na hela ya TCU 20000 na 5000 ya serikali ya wanafunzi walioshindwa kututetea tumesikia tu udomasana daruso ya udsm lakini nyinyi mkaa kimya yetuyetua tuwatuwapeiwalitutetea nyinsa
*Mwisho* kukabidhi kadi zetu za ccm na za ndugu zetu kama vile mama, baba mjomba shangazi kaka dada na nyinyink kwa mwenyekiti mpya atakae chaguliwa ili kuonyesha maumivu yetu na ndugu zetu kwa unyanyasaji huo tuliofanyiwa.

Vile kuiomba serikali kuturudisha udom ili tumalizie masomo yetu ili tusiwe tumepoteza mda bure maana tumefukuzwa sisi ni kwa sababu ya walimu wetu kudai mshahara yao sio kweli sisi tulikuwa ******.

Special diploma wote 7000 tunaomba tukutane dodoma tarehe 22 ili tujue hatma yetu tarehe 23 July Kwenye mkutano mkuu wa ccm asubuhi na mapema.

UMOJA NI NGUVU

By uongozi
Humo kwenye nyota nyota ni maneno gani yameondolewa? Au ni matusi? Maana kuna neno alitamka rais ambalo kinyiume chake ni Kipanga siku hizi ukiliandika linawekewa nyota nyota. Sasa neno alilolitamka rais hadharani inakuwaje lionekane halifai? Hii si ni sawa na kumsuta rais? Acheni liandikwe hivyo hivyo kama alivyolitamka yeye. Sasa hata jina la yule msichana nalo eti linawekewa nyota wakati ntu yupo na jina lake ni zuri tu na sio tusi?
 
Kumbe nauli ya kuchezea wanayoee?

Sasa ole wao tusikie wanajiuza tena.
 
Kama mtu alikupa nafasi pasipo kustairi yaani hukupaswa kupewa ns ameamua kuichukua unapiga kelele za nini?
Ninawahakikishia mkienda dodoma mnakwenda kuongeza majanga zaidi, hao wazazi wenu watauza mpaka nyumba kuwawekea dhamani na kulipia ghalama za matibabu, jaribuni mtaona.
Mbona huilaumu serikali iliyosababisha haya bali unasifia hii inayorekebisha utafikir wapinzani ndio walikuwa wanaongoza nchi, idiota. Hao waliowapa nafasi watu wasiostahili Mbona huwasemi? Hao wanafunzi wangefuata utaratbu wa kawaida leo wangekuwa wapi? Think acha ushabiki mi nakipenda hcho chama chako kuliko wewe, kunapokuwa na kosa jifunze kukubali.
 
Binafsi siamini kama itatokea hili kusanyiko. Siamini!
Maneno yana impact kuliko hata kwenda kabisa. Utakuta siku hiyo polisi wanaandaa silaha nzito, magari ya kuwasha, na hata kukodi polisi wengine kutoka mikoa jirani. Harafu vijana hawaji. Nani ataondoka na hasira.
 
Mh kwenye kurudisha kadi kumbe mlienda kichama kwaiyo mlipangwa wote ccm duh haya kumbe wenzenu ampigwi mabimu nendeni tu nyie ndugu
 
Duh shughuli pevu Dodoma . Wengine wamemwaga ugali wengine mboga, ugoko - chuma
 
Back
Top Bottom