fikirakali
Member
- Sep 15, 2014
- 15
- 18
Je, huu ni ubunifu au kuwakomoa wazazi? Kinachoendelea katika shule ya Sekondari Mbande ni kitu cha kutizamwa kwa Jicho la kipekee kwa kuwa kina madhara yake na kisipozungumzwa na kutolewa maamuzi na mamlaka kitaleta shida.
Kumeibuka mtindo wa kuwatoza wanafunzi matofali matatu na kuendelea kulingana na makosa ya kiuanafunzi kama vile kuchelewa, kutokusanya kazi au kutokumaliza kazi za darasani. Wakati naambiwa jambo hili na mtoto wangu anaesoma katika shule hiyo nilichukulia kuwa utani. Nilikuja kuamini baada ya kujionea mwenyewe nilipofika shuleni hapo mmoja wa waalimu akimwambia mwanafunzi alete tofali tatu kwa kutokumaliza kazi ya darasani.
Swali langu kwa wanajamii anaetozwa tafali ni mwanafunzi au mzazi? Mwanafunzi atapata wapi pesa kununua tofali?
Mamlaka husika wanalijua hili? Je, wazazi tumeridhia haya?
Je kuna meongozo unaoruhusu adhabu za kishule kwa wanafunzi kulipwa kwa pesa?