Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Braza nimekueleza humu wengi ni walimu tegemea kupata upinzani. Huyo unayemjibu ni Mwalimu wa shule ya msingi.Kukimbia tatizo si kulimaliza, hapa ni mwazo wa kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika, haiwezekani mwanafunzi ashindwe kuandika kazi au akose swali mzazi ukanunue matofali, kuna adhabu za kufyeka nyasi, kuchimba mashimo, kudeki madarasa na vyoo, hill la mtoto kutozwa pesa haikubaliki
Mimi nachokueleza ni hivi mpigie simu huyo mwalimu au mfuate, mwambie hiko kitu hakipo utaona jinsi atavyokua mpole. Wanawafanyia hivyo wakijua hamuwezi kuuliza, Ila ukianza kuuliza watajua huyu ni mjanja kashtuka.