DOKEZO Wanafunzi wanaagizwa kupeleka matofali ikiwa kama adhabu wanapofanya makosa shuleni

DOKEZO Wanafunzi wanaagizwa kupeleka matofali ikiwa kama adhabu wanapofanya makosa shuleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hivi kazi ya shule ni nini? Kufundisha na kutumia akili au kutumia nguvu kusolve matatizo madogo badala ya kutumia akili?
Alafu utakuta mtu mnalalamika toto lake limemaliza shule lakini halijui nini cha kufanya tofauti na ajira, je kazi ya shule iko wapi hapo?
Huu ni mzunguko usioisha sababu hata walimu walipitia huko hivyo wanaona sawa tu, I wonder why watanzania ni waoga na wajinga kupitiliza.

Huu uzi unaonyesha majority ya akili mbovu za kitumwa za waafrica ni kutumia nguvu nyingi na akili zero.
Mwanangu simpeleki akasome shule za ajabu kama hizi.
 
Acha kulela watoto kama mayai kwann wachelewe shule? Sisi tumepitia hayo mpaka tukamaliza.
Sisi shule yetu ilikua nje ya mji kidogo sasa Mimi nilifyatuaga tofali 300 kisa tulitoroka saa 4 ijumaa!! Sasa wakati tunasepa na wanangu kumbe mkuu wa shule alituona akiwa kwenye boda boda, yeye muda huo akiwa ndo anaenda shule.

Akamkariri jamaa mmoja sasa j3 tumekaa class akaingia, akasema kuna majambazi ijumaa walitoroka waje mbele wote kabla sijawainua mwenyewe, tukakausha wahuni sasa yule aliyekuwa amekaririwa akainuliwa na kofi taja wenzako akabisha, yule ticha alikua anapendaga kusema "nimelikuta msituni hili jambazi" wakampeleka ofsin akatutaja huko.

Kwanza tulipigwa alafu tukaambiwa kesho mje na wazazi bila hivo hamna shule.. mwisho wa siku kila mtu alifyatua tofali 300 kama adhabu.
 
Je, huu ni ubunifu au kuwakomoa wazazi? Kinachoendelea katika shule ya Sekondari Mbande ni kitu cha kutizamwa kwa Jicho la kipekee kwa kuwa kina madhara yake na kisipozungumzwa na kutolewa maamuzi na mamlaka kitaleta shida.

Kumeibuka mtindo wa kuwatoza wanafunzi matofali matatu na kuendelea kulingana na makosa ya kiuanafunzi kama vile kuchelewa, kutokusanya kazi au kutokumaliza kazi za darasani. Wakati naambiwa jambo hili na mtoto wangu anaesoma katika shule hiyo nilichukulia kuwa utani. Nilikuja kuamini baada ya kujionea mwenyewe nilipofika shuleni hapo mmoja wa waalimu akimwambia mwanafunzi alete tofali tatu kwa kutokumaliza kazi ya darasani.

Swali langu kwa wanajamii anaetozwa tafali ni mwanafunzi au mzazi? Mwanafunzi atapata wapi pesa kununua tofali?

Mamlaka husika wanalijua hili? Je, wazazi tumeridhia haya?
Je kuna meongozo unaoruhusu adhabu za kishule kwa wanafunzi kulipwa kwa pesa?
Kawaida sana, nakumbuka shule niliyosoma primary kila siku lazima uende na jiwe, hapo una kidumu cha maji, mfagio, maua na kila jumatano lazima ubebe jembe na mbolea na mfuko wako wa madaftari uko pale pale
 
Mimi tofali nilizofyatua shuleni kwa utovu wa nidgamu zinajenga vibanda vitatu kama vile vya waziri mkuu endapo kama zikijengwa kwa kusimamishwa.
 
Hivi kazi ya shule ni nini? Kufundisha na kutumia akili au kutumia nguvu kusolve matatizo madogo badala ya kutumia akili?
Alafu utakuta mtu mnalalamika toto lake limemaliza shule lakini halijui nini cha kufanya tofauti na ajira, je kazi ya shule iko wapi hapo?
Huu ni mzunguko usioisha sababu hata walimu walipitia huko hivyo wanaona sawa tu, I wonder why watanzania ni waoga na wajinga kupitiliza.

Huu uzi unaonyesha majority ya akili mbovu za kitumwa za waafrica ni kutumia nguvu nyingi na akili zero.
Mwanangu simpeleki akasome shule za ajabu kama hizi.
Nahuwezi kuwa na mtoto kwa sababu nawewe ni mtoto bado unakula kwa wazazi wako
 
Ndiyo matokeo ya elimu bure
Kama hutaki adhabu kama hizi uwe tayari kulipia elimu, peleka private. Huko mwanafunzi hata kazi ya kufagia darasa hafanyi
 
Kama tofali zinajenga madarasa hamna shida ila kama mwalimu zake hapo kuna shida. Tuliosoma zamani tunakumbuka EK tulikuwa tunapigika hasa
 
Mimi niseme tu ukweli isingekua adhabu za shuleni na mzazi kuwa na mimi sambamba kwenye kutengeneza nidhamu !! Ningekua mtu wa ovyo sana! Nisingekua hapa

Kwenye kulea watoto tumia njia zote bakora kiasi, ushauri wa kutosha na adhabu za kumjenga !!
Halafu ukiwa maskini ,umeshindwa kuwapa watoto maisha bora basi , komaa na nidhamu yao wawe watu wa kueleweka maishani !! Watakusifu baadae
 
mie nadhani adhabu zinazotolewa shuleni ni sehemu ya mafunzo kwaajili ya kumuandaa mwanafunzi na kuyakabili maisha yake ya mbeleni,yaani ni sehemu ya kujifunza stadi za kazi,akichelewa akapewa adhabu ya kulima shamba hapo ni sawa maana anajifunza kulima,yawezekana nyumbani kwao hata hajawahi kushika jembe lakini shule atajifunza na atalishika,hii inaenda sambamba na kazi zote za mikono kama kufyatua tofali n.k,lakini unapomtoza fedha ni dhahiri kuwa humsaidii ujuzi wowote zaidi sana utamsukuma ajifunze uongo na wizi ili aipate hiyo hela,waalimu wa siku hizi hata hawareason kwenye adhabu wanazotoa,zamani ukipewa adhabu huruhusiwi hata kupata msaada toka kwa wenzio lengo la waalimu lilikua ujifunze kitu kitachokusaidia in your future life,lakini naona humu wapingaji ni wengi bila hata kuelewa maana ya adhabu.
 
Nyie vijana wa siku hizi ndo maana mnakuwa mashoga. Tofali 5 tu unalalamika na kuja anzisha uzi? Kama hutaki hama hiyo shule. Mi nawapongeza sana walimu wa hiyo shule kwa kujenga nidhamu na kugawa ujuzi. So mwanafunzi achague kufyatua au kununua ni juu yake. Na awe na nidhamu pia. Hapo hata hamu ya kuwa shoga inamuisha. Nyie mmekuwa nyolonyolo sana mnajiona kama wanawake na mwishowe ndo mnaliwa.
 
Je, huu ni ubunifu au kuwakomoa wazazi? Kinachoendelea katika shule ya Sekondari Mbande ni kitu cha kutizamwa kwa Jicho la kipekee kwa kuwa kina madhara yake na kisipozungumzwa na kutolewa maamuzi na mamlaka kitaleta shida.

Kumeibuka mtindo wa kuwatoza wanafunzi matofali matatu na kuendelea kulingana na makosa ya kiuanafunzi kama vile kuchelewa, kutokusanya kazi au kutokumaliza kazi za darasani. Wakati naambiwa jambo hili na mtoto wangu anaesoma katika shule hiyo nilichukulia kuwa utani. Nilikuja kuamini baada ya kujionea mwenyewe nilipofika shuleni hapo mmoja wa waalimu akimwambia mwanafunzi alete tofali tatu kwa kutokumaliza kazi ya darasani.

Swali langu kwa wanajamii anaetozwa tafali ni mwanafunzi au mzazi? Mwanafunzi atapata wapi pesa kununua tofali?

Mamlaka husika wanalijua hili? Je, wazazi tumeridhia haya?
Je kuna meongozo unaoruhusu adhabu za kishule kwa wanafunzi kulipwa kwa pesa?
Miaka ya nyuma huko tulikuwa tunapiga tofali za shule kipindi cha likizo ,sio kama adhabu,ilikuwa assignment
 
Humu wengi ni walimu, tegemea kupingwa kwa ulichosema. Wewe cha kufanya nenda hapo shuleni au mpigie simu Mwalimu muonye kwahilo alilofanya. Utaona anakuwa mpole na samahani atakupa. Ila mkikaa kimya basi mtajenga nyumba bila kujua
Hapa sasa umenipa mwanga kumbe ni Waalimu!, maana nilikua nasoma comments huku nimebaki kinywa wazi, utumwa wa fikra hauwezi kuisha Tanzania halafu ndio tuna ndoto za kufika Dunia ya kwanza,
Mawazo finyu sana hawaangalii vitu kwa jicho la tatu,

Mtoto akifanya kosa ukamwambia alete Tofali na yeye hataki nyumbani wajue si ndio mwanzo wa kua mwizi au afanye uhuni ili apate pesa ya kununua hizo tofali,

Haya kosa la Mtoto kwanini Mzazi wake atoleshwe Pesa za kununua Tofali? Huyo Mzazi ana mangapi yanayomsibu na Tofali tena!!

Hiyo Tabia yapaswa kukemewa haijalishi ipo Shule nyingi (Shule nilizosoma sikuwahi kukumbana na hayo mauza uza) na haijalishi kwa kua wewe Mtu mzima uliwahi kupitia hayo basi kila kizazi kipitie,
Tubadilike.
 
Hivi kazi ya shule ni nini? Kufundisha na kutumia akili au kutumia nguvu kusolve matatizo madogo badala ya kutumia akili?
Alafu utakuta mtu mnalalamika toto lake limemaliza shule lakini halijui nini cha kufanya tofauti na ajira, je kazi ya shule iko wapi hapo?
Huu ni mzunguko usioisha sababu hata walimu walipitia huko hivyo wanaona sawa tu, I wonder why watanzania ni waoga na wajinga kupitiliza.

Huu uzi unaonyesha majority ya akili mbovu za kitumwa za waafrica ni kutumia nguvu nyingi na akili zero.
Mwanangu simpeleki akasome shule za ajabu kama hizi.
Upo sahihi kabisa,
Lishe duni inadumaza akili za wengi wanashindwa hata kujua haki zao ni zipi na wajibu wao ni upi,

Yaani kwa kua Mzazi alitembea kilomita 10 kwenda shule basi anataka na Mtoto wake atembee hivyo hivyo badala ya kupambana Mtoto wake asipitie aliyopitia.
 
Heri wanaoadhibiwa kuleta cement au bati au nondo.

Hizo tofali mara nyingi huwa zinaibwa kwenye site za watu jirani na shule hizo.
 
Kuna muhuni mmoja alikuwa akitaka kupigwa anamuhonga mwalimu 2,000 mwalimu anamuacha
 
Wewe lazima una mtindio wa ubongo, jamii kustaarabika ni ngumu sana kama mtu unaona hizi adhabu ni sahihi.
Ukimlegeza sana mtoto jiandae kuwa choko baadae....hizo ni Kaz za kawaida sana
 
Back
Top Bottom