DOKEZO Wanafunzi wanaagizwa kupeleka matofali ikiwa kama adhabu wanapofanya makosa shuleni

DOKEZO Wanafunzi wanaagizwa kupeleka matofali ikiwa kama adhabu wanapofanya makosa shuleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Badala kujenga hoja serikali iweke miundombinu ya maji mashuleni, wewe unashabikia watoto kubeba vidumu na kuni!

Tate umepotoka
Serikali gani hiyo ya kuweka miundombinu ya maji mashuleni kirahisi tu! Kwanza watoto wa hao viongozi wenyewe wa serikali wanasoma shule za private!! Lini wataguswa na matatizo lukuki ya shile za st. Kayumba!

Hao walimu wanaobuni hizo adhabu za kulipia matofali 3 siyo wajinga! Wanafanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kuwasadia hao watoto, na pia serikali yako iliyo wekeza nguvu kubwa kwenye siasa, badala ya elimu ya uhakika, nk.
 
Kuna wakati mmoja tuliambiwa na mwalimu wetu kuwa kwa kila siku moja mwanafunzi atakayochelewa kuripoti shule basi kufyatua tofali hamsini zitamhusu.

Na nilichelewa kwa siku 14, so tofali 700 zilinihusu.

Tulikuwa wengi tuliochelewa, tukafyatua tofali za kutosha, matanuri yakainuliwa na kuchomwa hadi tofali kuiva.

Eneo la kujenga vyumba vya madarasa likaandaliwa, tukapakua tanuri na kupeleka zile tofali site.

Hadi naondoka pale shule vyumba vya madarasa mawili vilikuwa vimefika level ya lintel. Hadi sasa vilishakamilika na vinatumika na wadogo zetu.

Adhabu kama hizi za kupeleka tofali huwa zinaamuliwa kwenye vikao vya wazazi ili kuimarisha nidhamu za wanafunzi shuleni.

Na mwanafunzi apewapo adhabu kama hizi mara zote huwekwa utaratibu wa mawasiliano baina ya mwalimu na mzazi/mlezi wa mwanafunzi husika ili mzazi awe na taarifa ya kile kinachoendelea. Hii husaidia sana mtoto kuonywa shuleni na nyumbani pia.

Aidha, wazazi/walezi wengi ambao hupenda kulalamikia adhabu kama hizi ni wale ambao huwa hawahudhurii vikao vya wazazi kwenye shule zetu, hasa hizi za St. Kayumba.

NB. Tusifuge watoto ila tulee watoto.
 
Nahuwezi kuwa na mtoto kwa sababu nawewe ni mtoto bado unakula kwa wazazi wako
Wow! This is just so Dumb!
Hata kama ningekuwa mtoto, Je watoto hawakui mpaka nao kuja kuwa na watoto?

Hii ndio thinking capacity ya teacher, I'm not surprised.
Not at all.
 
Serikali gani hiyo ya kuweka miundombinu ya maji mashuleni kirahisi tu! Kwanza watoto wa hao viongozi wenyewe wa serikali wanasoma shule za private!! Lini wataguswa na matatizo lukuki ya shile za st. Kayumba!

Hao walimu wanaobuni hizo adhabu za kulipia matofali 3 siyo wajinga! Wanafanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kuwasadia hao watoto, na pia serikali yako iliyo wekeza nguvu kubwa kwenye siasa, badala ya elimu ya uhakika, nk.
Sawa, lakini watoto kubeba madumu na mafurushi ya kuni sio jambo la faraja kama unavyolifurahia.

Kama inafanyika, ni kwa sababu tu hakuna namna, lakini HAIFURAHISHI kama unavyotuaminisha TATE.
 
Zamani tulikuwa tunapewa adhabu ya kuleta kuni.

Cha msingi hiyo adhabu isimhusishe Mzazi. Kama wametathmini wakaona kuwa mtoto atapata hayo matofali bila msaada wa Mzazi basi haina shida. Kinyume na hapo inakuwa kumwadhibu mzazi na siyo Mtoto.
 
Tofali zinakusaidia nini mwalimu?
Hazinisaidii chochote, bali zinatumika kwa ujenzi wa mazingira (kutengeneza bustani) kwa manufaa ya watoto wenu.

Faida ya hii adhabu...mwalimu hajichoshi kutumia nguvu, mtoto haumizwi kwa viboko
Ila maumivu kwa mzazi na hii pia inawakumbusha wazazi wajibu wa kulea vijana wenu.
 
Back
Top Bottom