Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wanafunzi wakilazimisha kuingia kwenye gari konda akiwazuia
Pamoja na kuchangia kiasi cha sh. 200 na kusisima huku wengine wakibanwa sana na watu wazima waliosisima pia kwenyehayo magari bado hata kupata chansi ya kuingia kwenye hayo magari imekuwa kizungumkuti kwao, makondakta wamekuwa wakiwasukuma wasipande huku wakiwatolea lugha chafu.
Napata mashaka kama kulikuwa na mjadala baina ya wamiliki wa daladala na wawakilishi wa madereva na makondakta wakati wa maamuzi ya kupanga nauli hiyo ya 200 kwa wanafunzi maana kwa jinsi makondakta wanavyowafanyia wanafunzi ni kama walipewa amri na serikali kuwa mtawabeba tu bila wao kuridhia na ivyo kukubali kishingo upande na wao wanalipiza kwa kuwanyanyasa wanafunzi.
Kama yalikuwa makubaliano kuna namna yoyote Serikali inafanya ufatiliaji wa kuona hawa wanafunzi wanatendewa nini? Kama 200 imepitwa na wakati je, wamefikiria nini kuweza kuwanusuru wanafunzi? Au mpaka siku mwanafunzi afie kwenye daladala kwa kusukumwa na kuanguka na kuingia kwenye tairi wakati dereva akikimbiza gari ili wanafunzi wasipande ndio tufikirie upya jambo hilo?
Wapo baadhi wanawachukua wanafunzi wawili au watatu huku wakilalamika, na wapo wanaowaambia ili wapande inabidi wawe na nauli za watu wazima, ila kuna walio wengi utasikia konda ondoa gari hii sio gari ya shule hatubebi wanafunzi, na wanafunzi wakisogelea gari basi husukumwa huko na gari likaondoka.
Wanafunzi wakimbembeleza konda awaruhusu kuingia kwenye daladala
Baadhi ya athari wanazokutana nazo wanafunzi kutokana na kukataliwa na makondakta.
1. Wengi wanachelewa shuleni au nyumbani kwa kukaa muda mrefu vituoni bila kupata usafiri kwa kuwa magari mengi yanawakataa kuwabeba.
2. Kuadhibiwa na Walimu wanapofika shuleni.
3. Mabinti wanarubuniwa kwa kupewa lifti kwenye magari ya watu binafsi.
4. Kupoteza morali ya kusoma kutokana na kusukumwa na kutukanwa na makondakta.
5. Kufika wakiwa wamechoka hoi kutokana na kukimbizana na kuwania magari ambayo mengi yanawakataa ivyo wanaathirika kisaikolojia.
Ushauri wangu yafanyike haya:
Daladala zitakazokubali kubeba wanafunzi zilipe kodi nusu au baadhi ya gharama kama ushuru wa stendi ili kuwafidia mahali wanapoona panaungua wakibeba wanafunzi.
Serikali iwaulize wamiliki wa daladala watakaokuwa tayari kubeba wanafunzi, kwenye kila njia, labda daladala kuanzia 3 hadi 5 inategemea na wingi wa watu eneo husika, Wawe wanapakia level seat halafu ile sehemu ambayo abiria wanasimama wasipande watu wa kawaida zaidi ya wanafunzi tu ili kuweza kuwabeba kwa wingi.
Daladala hizo ziongezewe mkanda wa njano kuonesha zitabeba na wanafunzi. Sheria iwatake wabebe wanafunzi asubuhi na jioni kwa gharama ya sh. 200.
Wanafunzi wakikimbiza gari baada ya konda kuwaacha bila kuwabeba!