Wanafunzi wawili wafariki kwa kukosa hewa wakitoa maharage kwenye pipa

Wanafunzi wawili wafariki kwa kukosa hewa wakitoa maharage kwenye pipa

Mungu awalaze mahali pema.
Kuna asilimia kubwa hao marehemu waliingia huko kwa lengo la kujificha, maisha ya boarding wanafunzi wengi wanawaza kujificha, kukweka kazi au adhabu.
 
Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye tenki la kuhifadhia maharage.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye tenki hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.

“Wanafunzi hao wote wana umri wa miaka 17, na uongozi wa shule umesema wote walifariki baada ya kuingia kwenye tenki kwa ajili ya kutoa maharage ya kupeleka stoo kwa ajili ya kupika,” amesema.

Ameongeza kuwa “Kwa taarifa tuliyoipata shuleni ni kwamba wanafunzi hao walipanda kwenye pipa hilo kwa kutumia ngazi na kisha kutumbukia ndani kutoa maharage na alianza kuingia mmoja, halafu akaanza kupiga kelele ndipo mwenzake akaingia kwa ajili ya kumuokoa lakini walikosa hewa na hadi kugeuza pipa kutolewa walishafariki,” amesema.

“Hapa inaonekana kuna uzembe, maana kama shule ina mpishi, kwa nini wanafunzi waingie kwenye pipa kwa ajili ya kutoa maharage kupeleka stoo? Alihoji mwenyekiti huyo na kueleza kuwa, tayari vyombo vya usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya walifikaa eneo la tukio

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori kuzungumzia tukio hilo, amesema atalizungumzia baadaye.

Chanzo: Mwanachi
Picha ya tenki tafadhali
 
Maskini wanafunzi! Walazwe pema na kwa Amani.

Tukio kama hili lingeweza epukika kama wahusika wangefuata 'taratibu au kanuni ya kuingia kwenye nafasi funge' yaani 'Entering confined space safety procedure'.

Elimu kwa wananchi inabidi kutolewa ipasavyo na taasisi husika kuhusiana na vihatarishi vinavyotuzunguka katika sehemu zetu za kazi na kadhalika katika maisha yetu ya kawaida.

Baadhi ya vyanzo vya vifo vitokanavyo na ukosefu wa hewa ya oksijeni ni pamoja na:
-Nafasi funge au 'confined space'
-Mashimo na mitaro funge ya maji taka
-Majiko ya mkaa
-Migodi ya chini ya ardhi au 'underground mines'

Wananchi wakielemishwa vyema hakika vifo vya aina hii vitaepukwa au kupungua kwa kiasi kikubwa.
 
Bila picha ya pipa tutajiukliza sana, pipa limeua kwa mda mfupi sana au kulikuwa na kitu zaidi ya kukosa hewa, yaani mmoja ameingia akaanza kupiga kelele mwenzake akaiingia kwenda kumuokoa wote wamepoteza maisha, walikaa mda gani humo ndani ya pipa.
 
Nchi hii ngumu sana
Yaani hii nchi ni ngumu vibaya mno yaani mimi kama mzazi nilipe ada alafu bado nisikie mtoto wa miaka hiyo anafanyishwa kazi ambazo hata mfanyakazi hafanyi nitatoa mtu roho, wachagga acheni ukuda wa kutumikisha wanafunzi kwenye shule zenu za kikatoliki.
 
Mungu awalaze mahali pema.
Kuna asilimia kubwa hao marehemu waliingia huko kwa lengo la kujificha, maisha ya boarding wanafunzi wengi wanawaza kujificha, kukweka kazi au adhabu.
Wasoma Heading.
 
Back
Top Bottom