reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,203
- 28,789
Yaani tunapenda mnoooWalimu wanapenda sana kutuma watoto
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani tunapenda mnoooWalimu wanapenda sana kutuma watoto
NawajuaYaani tunapenda mnooo
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]Nawajua
Hajasema "my classmayes" amesema "clssmates" yaani wao wako darasa moja.Yan we kila mtu umesoma naye 😆
Vumbi la maharage au wamezama kwenye maharage ?? Sijawahi kusimama kwenye maharage, sijui surface stability ya maharage.Na vumbi la maharage huchelewi....ni chap! RIP wanangu
Swali kwa aliyesikia kelele za mwanafunzi wa kwanza.Bila picha ya pipa tutajiukliza sana, pipa limeua kwa mda mfupi sana au kulikuwa na kitu zaidi ya kukosa hewa, yaani mmoja ameingia akaanza kupiga kelele mwenzake akaiingia kwenda kumuokoa wote wamepoteza maisha, walikaa mda gani humo ndani ya pipa.
Mkuu nilitamani sana kuona Comment kama hii.Maskini wanafunzi! Walazwe pema na kwa Amani.
Tukio kama hili lingeweza epukika kama wahusika wangefuata 'taratibu au kanuni ya kuingia kwenye nafasi funge' yaani 'Entering confined space safety procedure'.
Elimu kwa wananchi inabidi kutolewa ipasavyo na taasisi husika kuhusiana na vihatarishi vinavyotuzunguka katika sehemu zetu za kazi na kadhalika katika maisha yetu ya kawaida.
Baadhi ya vyanzo vya vifo vitokanavyo na ukosefu wa hewa ya oksijeni ni pamoja na:
-Nafasi funge au 'confined space'
-Mashimo na mitaro funge ya maji taka
-Majiko ya mkaa
-Migodi ya chini ya ardhi au 'underground mines'
Wananchi wakielemishwa vyema hakika vifo vya aina hii vitaepukwa au kupungua kwa kiasi kikubwa.
Wasomi wa nchi hii hawana uwezo wa kufanya kuweka tahadhari ya kuwahami watu mpaka wafe waumie hapo serikali utaisikia heti tunatoa lambi lambi na kusimamia mazishi na kuandaa sehemu salama ya kuhifadhia maharagwe fiweeeeWanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye tenki la kuhifadhia maharage.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye tenki hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.
“Wanafunzi hao wote wana umri wa miaka 17, na uongozi wa shule umesema wote walifariki baada ya kuingia kwenye tenki kwa ajili ya kutoa maharage ya kupeleka stoo kwa ajili ya kupika,” amesema.
Ameongeza kuwa “Kwa taarifa tuliyoipata shuleni ni kwamba wanafunzi hao walipanda kwenye pipa hilo kwa kutumia ngazi na kisha kutumbukia ndani kutoa maharage na alianza kuingia mmoja, halafu akaanza kupiga kelele ndipo mwenzake akaingia kwa ajili ya kumuokoa lakini walikosa hewa na hadi kugeuza pipa kutolewa walishafariki,” amesema.
“Hapa inaonekana kuna uzembe, maana kama shule ina mpishi, kwa nini wanafunzi waingie kwenye pipa kwa ajili ya kutoa maharage kupeleka stoo? Alihoji mwenyekiti huyo na kueleza kuwa, tayari vyombo vya usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya walifikaa eneo la tukio
Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori kuzungumzia tukio hilo, amesema atalizungumzia baadaye.
Chanzo: Mwanachi
haya mambo ya kuwashirikisha wanafunzi kwenye mambo ambayo kimsingi hawatakiwi kufanya ni uzembe wa walimu kuruhusu wanafunzi washiriki kazi ambazo tayari kuna mfanyakazi wake.
Nilitaka kusema nikaogopa kushushuliwa.Yan we kila mtu umesoma naye 😆
Siwaelewi km Mimi Ndo mwenye Mtoto ama zao ,ama zangu aseehhMzazi hapo unawaelewaje wahusika?