reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,203
- 28,789
Duhhh....Sasa kwanini wanaruhusu watu waingine jamani....[emoji3064][emoji3064][emoji3064]Hayo mapipa yametengenezwa kuzuia hewa isiingie ili wadudu wala nafaka wasi survive
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duhhh....Sasa kwanini wanaruhusu watu waingine jamani....[emoji3064][emoji3064][emoji3064]Hayo mapipa yametengenezwa kuzuia hewa isiingie ili wadudu wala nafaka wasi survive
Elimu ya tahadhariDuhhh....Sasa kwanini wanaruhusu watu waingine jamani....[emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Uongozi wa shule uchukuliwe hatuaWanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye tenki la kuhifadhia maharage.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye tenki hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.
“Wanafunzi hao wote wana umri wa miaka 17, na uongozi wa shule umesema wote walifariki baada ya kuingia kwenye tenki kwa ajili ya kutoa maharage ya kupeleka stoo kwa ajili ya kupika,” amesema.
Ameongeza kuwa “Kwa taarifa tuliyoipata shuleni ni kwamba wanafunzi hao walipanda kwenye pipa hilo kwa kutumia ngazi na kisha kutumbukia ndani kutoa maharage na alianza kuingia mmoja, halafu akaanza kupiga kelele ndipo mwenzake akaingia kwa ajili ya kumuokoa lakini walikosa hewa na hadi kugeuza pipa kutolewa walishafariki,” amesema.
“Hapa inaonekana kuna uzembe, maana kama shule ina mpishi, kwa nini wanafunzi waingie kwenye pipa kwa ajili ya kutoa maharage kupeleka stoo? Alihoji mwenyekiti huyo na kueleza kuwa, tayari vyombo vya usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya walifikaa eneo la tukio
Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori kuzungumzia tukio hilo, amesema atalizungumzia baadaye.
Chanzo: Mwanachi
Uko sahihi The622.Mkuu nilitamani sana kuona Comment kama hii.
Serikali na wadau wengine wa usalama wamejitahidi sana kutoa elimu shuleni juu ya Usalama barabarani ,na kwa kiasi kikubwa mwanga umeonekana.
Lakini ni muda Sasa kutoa elimu zaidi juu ya elimu ya Usalama mahala pa kazi(Safety in the Workplace).
Shule ni eneo lenye Vihatarishi vingi sana ambavyo visivyodhibitiwa vinaweza kuleta madhara makubwa si tu kwa wanafunzi,Bali hata kwa walimu na wafanyakazi wengine wanaozunguka eneo husika.
Natoa pole kwa wazazi na walimu waliopoteza vijana wetu na nguvu kazi kwa taifa.
Hili ni jukumu la Kila mmoja kujielimisha na kuwasaidia wengine.
Hata usiyogope mashushu hayauwi,ndio yanakupa ujasiriNilitaka kusema nikaogopa kushushuliwa.
Unajifanya mjuaji kishenzi!Siwaelewi km Mimi Ndo mwenye Mtoto ama zao ,ama zangu aseehh
Shule Ina wapishi,wafanyakazi how comes wamtume mwanafunzi hukooo....
Walimu tuna uzembe mnooo!
Haya sawaHata usiyogope mashushu hayauwi,ndio yanakupa ujasiri